The House of Favourite Newspapers

Rais Magufuli: Nawaomba Tutulie Juhudi za Uokoaji Zinaendelea

Rais Dkt. John Magufuli ametuma salamu za rambirambi na pole kutokana na ajali ya kuzama kwa Kivuko cha MV Nyerere kichachofanya safari zake kati ya Bugorora na Ukara katika Ziwa Victoria kilichozama jana Alhamisi, Septemba 20, 2018 mchana.

 

Kupitia kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais- Ikulu, Gerson Msigwa, Rais Magufuli ametoa salamu hizo jana usiku kwa njia ya simu kupitia Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wakati wa taarifa ya habari.

 

“Rais anatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki waliofikwa na ajali. Rais anaomba Watanzania kuwa watulivu wakati juhudi za uokoaji zinaendelea na baadaye Serikali itaweza kutoa taarifa ya nini kitakachoendelea.”

 

“Nimeshtushwa na kusikitishwa sana na ajali ya MV Nyerere, nawapa pole wote waliopoteza jamaa zao na nawaombea wote walionusurika kupona haraka, kwa wakati huu nawaomba tutulie wakati juhudi za uokoaji zinaendelea” – Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

 

KWA mujibu wa HABARI ZA MIKOANI kutoa TBC 1, imeelezwa kuwa mpaka leo asubuhi, waliookolewa wakiwa wamepoteza maisha idadi yao imeongezeka na kufikia 79 huku majeruhi wakiwa ni 37.

 

TAZAMA VIDEO MIILI IKIOKOLEWA

Comments are closed.