The House of Favourite Newspapers

Yanayojiri Kesi ya Godbless Lema Arusha Leo… Lowassa, Sumaye Waibuka Mahakamani

Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Jonathan Lema akishuka kwenye gari kuingia mahakamani.

ARUSHA: Mahakama Kuu Kanda ya Arusha leo Machi 3, 2017 inatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu maombi ya dhamana ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) baada ya kuwekwa kizuizini kwa takribani miezi minne tangu Novemba 2 mwaka jana alipokamatwa.

Viongozi mbalimbali wa Chadema wakiongozwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Vicent Mashinji, Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Edward Lowasa, Waziri Mkuu Msaatafu Sumaye na Meya wa Jiji la Arusha Mjini Kalisti Lazaro wakiwa mahakaman .

Mnamo Feb 27, Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ikiongozwa na majaji watatu, iliyokaa Arusha ilitupilia mbali Rufaa zote mbili zilizofunguliwa na Serikali dhidi ya maamuzi ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kuhusu pingamizi la dhamana ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Jonathan Lema.

Mahakama hiyo, ilitoa maelekezo kuwa jalada la kesi hiyo lipelekwe Mahakama Kuu ili kuendelea na mchakato wa kumpatia dhamana katika kesi inayomkabili kwani hakuna hoja ya msingi kwa rufaa iliyokatwa na mawakili wa serikali.

Majaji walisoma mapingamizi ya mawakili wa serikali bila kuona tija yoyote ya kisheria, hivyo wakatoa amri kwa Mahakama Kuu kulishughulikia suala la Godbless Lema haraka.

Naibu Katibu Mkuu Chadema John Mnyika, pamoja na Viongozi mbalimbali wakiwa mahakamani leo.

Tutaendelea kukujuza kila kinachojili.

Comments are closed.