The House of Favourite Newspapers

Siwema Anangwa Kumpotezea Mwanaye

Siwema

Na MUSSA MATEJA| GAZETI LA IJUMAA| STAR MIX

MREMBO Siwema Edson aliyezaa na msanii wa muziki Bongo, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego   ’ amenagwa na watu wake wa karibu baada ya kutua Bongo kisha kutotaka kumuona mwanaye.

Siwema

Chanzo chetu cha kuaminika kimedai kuwa, Siwema ‘Mama Edson’ yupo mjini lakini kila alipokuwa akishauriwa kwenda kumuona mwanaye amekuwa akipotezea. “Yaani jamani Siwema sijui ni mwanamke wa aina gani, tangu alivyombwagia Nay mtoto hajawahi kumuona, hivi anaweza kusema alipata uchungu kweli wakati wa kujifungua?” alihoji mtoa habari huyo ambaye ni rafi ki wa Siwema.

Katika kujua ukweli wa habari hii, mwandishi wetu alimtafuta Siwema kupitia simu yake ya mkononi  ambapo alipoulizwa sababu za kutokwenda kumuona mwanaye alisema:

“Siyo kwamba sitaki kumuona mwanangu, napenda sana lakini sasa kila nikimpigia simu Nay na kumwambia kuhusu hilo, kunakuwa na danadana nyingi sasa na mimi siwezi kulazimisha mambo.”

Comments are closed.