The House of Favourite Newspapers

‘HUMANITY AUCTION FOR CHILDREN FOUNDATION’ YAGAWA MSAADA KWA WALEMAVU

Bi. Rahma akiongea na walemavu hao kabla ya kuanza kuwapa misaada hiyo (hawapo pichani).

TAASISI isiyo ya kiserikali ya Humanity Auction For Children Foundation ambalo lengo lake ni kuwasaidia walemavu wa aina mbalimbali ikiwemo viungo, vipofu, na maalbino leo imewapa msaada wa vitu mbalimbali walemavu hao kwenye hafla iliyofanyika Ukumbi wa Moramo uliopo Sinza-Makaburini jijini Dar.

Walemavu hao walipatiwa vitu mbalimbali vikiwemo kofia za kutembelea juani kwa albino, fimbo za vipofu, magongo ya kwapani na mkononi, viti vya magurudumu na misaada mingine.

Mmoja wa viongozi wa taasisi hiyo, Faidha Ally, akiongea machache katika zoezi la utoaji wa zawadi hizo.

Akizungumza baada ya kutoa misaada hiyo mwanzilishi wa taasisi hiyo Bi. Rahma Mohammed amesema taasisi yake imepokea misaada hiyo kutoka Ubalozi wa Kuwait hapa nchini hivyo anahakikisha inawafikia walemavu hao kama lengo lilivyokusudiwa. Walemavu hao baada ya kupokea misaada hiyo walimshukuru Bi. Rahma pamoja na Ubalozi wa Kuwait kwa kuwatazama kwa jicho la huruma na kuwaombea Mungu azidi kuwazidishia.

Rahma na mwenyekiti wa taasisi hiyo, Rashid Mchujuko, wakimkabidhi fimbo ya kutembelea mwenyekiti wa Chama cha Wasioona Mkoa wa Dar es Salaam, Seif Jega (wapili kulia)
Mwenyekiti wa Chama cha Maalbino Manispaa ya Kinondoni, Leonard Kidole, akiwa na mzigo wa kofia za maalbino baada ya kukabidhiwa.
Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu wa Viungo Manispaa ya Kinondoni, Subira Semsimbazi, akiwa amekalia kiti cha magurudumu baada ya kukabidhiwa kiti hicho pamoja na magongo ya kutembelea.
Viongozi wa taasisi hiyo wakiwa vitini wakati mambo mengine yakiendelea.
Sehemu ya walemavu waliohudhuria hafla hiyo.

PICHA: RICHARD BUKOS / GPL   

Comments are closed.