The House of Favourite Newspapers

Huyu Naye..! Fuata Maelekezo-15

0

ILIPOISHIA RISASI JUMAMOSI:
“Kwa hiyo mume wangu unatakaje?” nilimuuliza nikimwangalia kwa macho ya kulegea. Niliyalegeza kwa makusudi kabisa.
Mara, nikamwona mwenzangu anafungua tai, anavua shati, anafungua mkanda wa suruali, mara…
TEMBEA NAYO MWENYEWE…

Ilikuwa saa tatu na nusu asubuhi, baba Rehema ndiyo aliondoka kwenda kazini maana ilibidi akaoge tena, ajiweke sawasawa ndipo atoke.
“Lo! Yaani mpenzi wangu umeshindwa kabisa kwenda kazini kwa sababu ya haya mambo?” nilimuuliza…
“Yaani jioni ni mbali sana kwangu. Ndiyo maana nimeamua kufanya hayo mambo kabla sijaenda kazini vinginevyo ningekuwa sina raha na kazi na ingekuwa ngumu sana kwangu leo.”
Ile anataka kutoka chumbani tu, mama Rehema akasukuma mlango, akaingia chumbani akiwa ameongozana na watu wengine wanne, akiwemo mwanamke mmoja…
“Leo nimekufumania baba Rehema, huniambii kitu hata kidogo,” alisema mama Rehema.
Mimi nilikimbilia chini ya kitanda lakini wakati nainama, baba Rehema akanishika huku akiniambia…
“Wala usikimbie.”
“Umefumaniwa bwana…”
“Umefumaniwa na mkeo leo…”
“Kumbe wewe ndiyo mchezo wako wa kulala na mahausigeli,” walisema wale wanaume wengine na kusababisha kelele chumbani mpaka ikawa kero…
Mimi nilikuwa sijavaa nguo nyingine zaidi ya kanga moja tu ambayo nayo ikawa inavukavuka mara kwa mara na kuivaa tena mpaka aibu.
Mama Rehema akanivaa, lakini baba Rehema akamzaba kofi moja tu, kule chini…
“Acha ujinga. Kwanza nyie nani kawapa kibali kuingia chumbani kwangu?” baba Rehema alikuja juu.
Bila kujali tai aliyovaa alianza kuwapiga makonde wote huku eti na wao wakisema wameitwa na mama Rehema kuja kumfumania mume wake…
“Nani anayejua huyu ni mke wangu kati yenu?” baba Rehema aliwauliza akiendelea kuwapiga, wakatoka mbio. Mama Rehema naye akatoka mbio.
Nilibaki na baba Rehema ambaye alikuwa akihema sana kwa kazi ya kuwapiga wale wafumaniaji wangu…

“Wapuuzi sana wale. Wanawezaje kuniletea ujinga wao hapa. Wamenifumania kwani wao ni akina nani? Hakuna hata mtu mmoja ninayemjua pale…eti umefumaniwa na mke wako leo…kenge wakubwa,” alilalama baba Rehema.
Wakati huo nilikuwa nimekaa kitandani huku nimejiinamia. Akanifuata, akanishika mkono na kunisimamisha huku akiniambia maneno ya kunibembeleza…
“Sweet usiogope, hana chake tena mama Rehema…we muone kama amechanganyikiwa tu…hivi unajua kwa nini nimekuwa nikimpuuza mara kwa mara?”
“Kwa nini?” nilimuuliza tena nikiwa na shauku kubwa ya kujua hilo alilolisema maana ni kweli hata mimi nimekuwa nikiwaza kwamba, baba Rehema anampuuza sana mke wake…

“Yule mwanamke ni kama changudoa tu,” alisema baba Rehema mpaka nikashtuka. Mimi ninavyojua changudoa ni mwanamke anayejiuza, sasa yeye anaposema mkewe ni kama changudoa ana maana gani!
“Kwa nini unasema hivyo?”
“Amekuwa akitembea na vitoto mtaani kwa sababu ya kutaka vijisenti…we najua hujui lakini huo ndiyo ukweli wa mambo.”
“Mh! baba Rehema kweli?”
“Ohoo! Nimeshamnasa zaidi ya mara tatu na vijanavijana wa mtaani. Sasa limama kama lile na vitoto wapi kwa wapi!”
Nilishangaa sana.

Tulikuwa tumesimama, baba Rehema akanibusu kwamba sasa anaondoka kwenda kazini…
“Baadaye mpenzi wangu, funga geti, mtu akigonga usifungue hadi ujue ni nani? Hata kama ni Rehema lazima ajitambulishe kwanza maana huyu dadapoa anaweza kurudi kwa staili nyingine,” baba Rehema aliniambia akiwa amemaliza kunibusu.

Nikasema moyoni kwamba kwa nini na mimi nisimbusu ili kumtakia kazi njema bwana! Nikambusu. Kwa sababu ya urefu wake, ilibidi nimshike shingoni ili kumwinamisha alipate busu langu kwa usahihi.
Kumbe kule kumwinamisha yeye akajisikia raha, si akanilazimisha kula denda tena…

“Mmm…nini bwana! Utachelewa kazini huko,” nilimwambia huku nikipisha midomo yangu pembeni.
Lakini wapi! Alinibana kwelikweli mpaka nikajikuta nalegeza masharti mimi mwenyewe…
“Mmm…mmm…” tulizama.

Kuja kushtuka, tupo kitandani tena. Moyoni nikasema kama nilimkatalia denda akalazimisha, sasa tuko kitandani, hawezi kunielewa kwa lolote lile. Tukaingia uwanjani na kuanza mchezo. Lakini ilibidi nimchojoe mavazi kwanza na kuyatupilia mbali bila kujali yatakunjika au vipi! Shauri zake mwenyewe.
Tukiwa tumeanza tu kucheza, tukasikia sauti nyingi zaidi ya zile za mwanzo kutokea sebuleni…
“Yuko wapi..? Yuko wapi huyo mwizi wa waume za watu?”
Tulishtuka wote, tukaangaliana  kwa macho ya wasiwasi. Naamini kila mmoja wetu alikuwa anajiuliza…
“Ina maana wamerudi tena?” aliuliza baba Rehema huku akitoka kitandani na hasira.

Nilimwona akivaa bukta, akafungua mlango wa kabati la nguo, akazamisha mkono kwenye nguo na kutoka na bastola…
“Jamila utaniletea chakula nikiwa magereza, nimechoka na udhalilishaji huu hapa nyumbani kwangu,” alisema baba Rehema huku akitoka kwa kasi…
“Mpenzi…mpenzi…baba Rehema,” niliita lakini hakunisikiliza. Na mimi nikiwa kwenye kanga yangu moja nikamfuata kwa nyuma, mbio, nikasikia paa..!
Je, unajua nini kiliendelea hapo? Usikose kusoma kwenye Gazeti la Risasi Jumamosi ijayo

Leave A Reply