The House of Favourite Newspapers

Huyu Naye…fuata Maelekezo – 08

0

ILIPOISHIA RISASI JUMATANO:

Kwa kweli chumbani kulikuwa mbali sana, wote tulijikuta palepale sebuleni tukizama kwenye denda sasa huku nikimshukuru sana baba Rehema kwa simu japokuwa nilikuwa sijaiona kwa macho zaidi ya boksi…

“Hivi kwa nini huyu Jamila hajafunga geti?” sauti ya mama ilisema huku ikishika mlango mkubwa wa kuingia sebuleni tulipo…

JIACHIE NAYO MWENYEWE…

Nilimsukuma baba Rehema akaangukia kwenye kapeti la manyoyanyoya, mimi nikaenda jikoni kwa haraka sana…

“He! Mwenzetu vipi tena?” mama Rehema alimuuliza mume wake, nikatega sikio kusikiliza atajibu nini? Je, atajua alikuwa na mimi?

“Nilikuwa nasimama kwenda chumbani, ghafla tumbo limenishika….daaa! Linakata kwelikweli…”

“He! Ni nini? Umekula nini kazini leo?”

“Nimekula kawaida tu asubuhi, chai na mkate tena vipande viwili.”

“Jamila…” aliita mama…

“Abee.”

“Hebu nisaidie tumkalishe baba Rehema kwenye kochi hapa,” alisema mama Rehema. Tukamshika huku na huku tukamuweka kwenye kochi kubwa…

“Au twende hospitali?” mama Rehema alimshauri…

“Hapana…hakuna haja. Naamini litatulia tu,” alijibu baba Rehema huku akiendelea kujishikashika tumbo.

“Basi ngoja nikakuletee maji ya moto,” alisema mama Rehema na kwenda jikoni akiniacha mimi na mume wake sebuleni.

Baba Rehema aliniangalia akaachia tabasamu laini, akasema kwa sauti ya chini sana…

“Tumesevu soo Jamila.”

Nilimkubalia kwa kutingisha kichwa nikiogopa kutoa sauti…

Moyoni nilijisemea kwamba laiti kama angejua kilichoendelea kati yangu na baba sijui ingekuwaje.

Wakati nikiwaza hivyo, baba alinibonyeza katika paja langu, wote tukatabasamu.

“Hebu kunywa maji haya baba Rehema. Wewe Jamila kaendelee na kazi zako,” alisema mama Rehema.

Niliendelea na shughuli zangu huku nikicheka mwenyewe kila wakati. Nilijiuliza maswali mengi sana kuhusu tukio tulilotaka kulifanya pale sebuleni…

“Hivi ni kwa nini sikuwaza kuhusu geti kubwa?”

“Je, endapo mama asingesema kuhusu kutofunga geti si ina maana angetufumania? Lo!”

*   *   *

Baba Rehema sasa alikuwa akiendelea vizuri na tumbo lake. Nilipika chakula, akaja kula akiwa amekaa na mke wake.

Lile boksi la simu lilikuwa kwenye kochi na hakuna aliyezungumzia licha ya kwamba, nilimuona mama Rehema kama mara mbili hivi akilishikashika.

Wakiwa wanakula, baba Rehema aliniita niende kwenye chumba cha kulia chakula. Kufika akasema…

“Lile boksi lina simu ya tochi, ni yako. Sasa mama Rehema atakusaidia kununua laini.”

Nilimwangalia mama Rehema, tukakutana jicho, wee! Jicho lilikuwa kali sana kama vile alitaka kunipasua kichwa…

“Nitakununulia siku nikipata pesa au kama una pesa zako za mshahara nipe nikakununulie,” alisema mama Rehema. Eti siku akipata pesa!

“Mama Rehema unasema siku ukipata pesa? Kwani laini ni shilingi ngapi?” baba Rehema aliuliza…

“Elfu mbili mia tano unapata.”

“Hiyo ndiyo mpaka siku ukipata fedha mama Rehema?”

Mama Rehema alisimama na kuondoka huku akiwa hajajibu swali la mume wake. Nilimwangaliwa kwa jicho la kumzodoa lakini yeye hakuniona.

“Mh! Huyu mama ana roho mbaya sijui kama nini! Hana lolote zaidi ya kutofurahishwa mimi kununuliwa simu na baba,” nilijisemea moyoni.

Baba alinipa boksi lenye simu nikaenda chumbani kuitoa. Nilikuwa nina laini yangu sijaitumia kama miezi miwili nyuma, nikaiweka ikafanya kazi.

Kitendo cha baba kuninunulia simu kilinifurahisha, nilibaini kweli alinijali na kunipenda.

Nilipofika sebuleni, nilimkuta baba Rehema lakini mama Rehema hakuwepo…

“Nimepata laini tayari, mama yuko wapi nimwambie?” nilimuuliza baba Rehema…

“Ametoka nje huko…nitajie namba zako,” aliniambia, nikamtajia. Akatuma meseji ya kunionesha namba zake.

*   *  *

Ilikuwa saa sita usiku, nilikuwa kitandani naongea na wazazi wangu mkoani, maana namba ya simu ya kaka yangu niliiandika kwenye karatasi na kokote ninakokwenda ninayo ili nikitaka kuwasiliana na baba au mama napiga hiyo.

Nilikuwa naongea na mama, nikasikia mlio wa meseji, nikamwambia mama nakata simu nitapiga baadaye.

Nilisoma meseji, ilitoka kwa baba Rehema. Unajua wakati namsevu kwenye simu yangu nilijiuliza mara mbilimbili nitumie jina gani kati ya Baba Rehema, Bosi au Mpenzi. Nikasevu Mpenzi wa Miye!

“Umelala wewe?” aliniuliza.

“Badooo!” nilimjibu. Lakini baada ya kumjibu nikajishtukia kwamba, nina uhakika gani kama ile meseji ilitoka kwake baba Rehema…

“Acha mlango wazi nakuja sasa hivi, usiwe na wasiwasi huyu mama Rehema amelala fofofo,” aliniambia.

“Njooo!” nilimwita moyoni nikasema potelea mbali kama mama Rehema ndiye aliyenitumia meseji…

“Basi nikukute tayaritayari, hakuna kupoteza muda,” aliongeza.

Nilitoka kitandani, nikafungua mlango na kuuacha wazi, nikachojoa nguo, nikarudi kitandani…

 Je, unajua nini kiliendelea hapo? Usikose kusoma kwenye Gazeti la Risasi Jumatano ijayo.

Itaendelea wiki ijayo siku ya Jumatano katika Gazeti la Risasi Mchanganyiko

Leave A Reply