The House of Favourite Newspapers

Huyu Ndo Kiumbe Mwenye Umri Mrefu Zaidi Aliye Hai

0

WAKATI mwingine kudra za Mungu hazichunguziki na hasa ukisikia kuna mnyama Kobe kafikisha umri wa miaka 189.
Kombe huyo anaitwa Jonathan ambaye ametajwa kuzaliwa mwaka 1832 ameweza kuvuka changamoto kibao za kafya na kiusalama zinazotokea duniani.

 

Wewe na mimi kama tunaogopa Ugonjwa wa Corona, Jonathan anatukumbusha jambo muhimu kwamba; “kila kitu kitapita.”
Maana yeye kafanikiwa kupita kwenye joto la vita za dunia, Mapinduzi ya Urusi, kawashuhuda marais 39 wa Marenikani, kawaona watawala saba wa Uingereza; sasa utamwamba nini maana hata mageuzi ya teknolojia mengi kayaona?

 

Kobe Jonathan, kutoka Saint Helena nchini Uingereza, ndiye mnyama wa ardhini ambaye yupo hai mwenye umri mkubwa zaidi duniani kwa sasa kulingana na kitabu cha Rekodi Duniani (Guinness World Records). Vita vya kwanza vya dunia (Jul 28, 1914 – Nov 11, 1918) Kobe Jonathan alikuwepo, vita vya pili vya dunia (Sep 1, 1939 – Sep 2, 1945), Kobe Jonathan alikuwepo.

Ameivunja rekodi Kobe Tu’i Malila, aliyekuwa akimilikiwa na Familia ya Kifalme, Tonga huko Uingereza ambaye alifariki mwaka 1966 akiwa na umri wa miaka 188.

 

Lakini jambo jema kwa Kobe huyo anayeishi Kisiwa cha mbali cha Mtakatifu Helena, Atlantiki Kusini kwa mujibu wa Kikundi cha Mtaalam wa Kobe cha IUCN wanakadiria kuwa Jonathan anaweza kuishi miaka mingi zaidi ijayo.

 

Ikubukwe kuwa, kobe huyo tayari amevuka kigingi cha umri wa wanadamu kuishi kwa kwa zaidi ya miaka 65. Takwimu zinaonesha kuwa, umri mkubwa uliothibitishwa kwa mwanadamu ni miaka 122 na siku 144, (1875–1997) aliyoishi Mfaransa Jeanne Calment na hivyo kumpa nafasi kobe huyo kuwa mnyama mwenye miaka mingi kuliko wote duniani.

 

Kumekuwa na rekodi nyingi zinazoonesha kuwa wanyama aina ya Kobe hasa kutoka Bara la Afrika wanaishi kwa miaka mingi.
Ingawa Jonathani anaishi nchi za mbali lakini mnyama huyo anadaiwa alitoka Afrika katika visiwa vya Ushelisheli katika Bahari ya Hindi na kwamba alipelekwa

kwa Mtakatifu Helena kama zawadi wakati huo akiwa na umri wa miaka kama 50 hivi. Ndiyo maana nimesema, kudra za Mungu za kuochwa tu, maana kuna kisa cha kobe mwingine aitwaye “Alagba” kutoka nchini Nigeria yeye aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 334.
Vipi umeanza kutamani ungezaliwa kobe ili uishi miaka mingi?

ACHA KUKUFURU WEWE!
@manyota_rich

 

 

Leave A Reply