The House of Favourite Newspapers

Huyu Nd’o Muuaji Aliyeua Wauaji Zaidi ya 70

0

IMEKUWA kwamba chaguo (choices) tunayochagua ndiyo yanatueleza tulivyo. Kuna msemo kwenye biolojia unaosema: ” Every major decision made human brain undergo a physical change over time” (kila uamuzi mkubwa ulimfanya binadamu kubadili maamuzi yake ya kimwili katika muda fulani) Lakini vipi kuhusu maamuzi ya mtu kuchagua maisha ya kuwa muuaji?

 

Watu waliochagua kuishi kama wauaji wapo na huyu ni muuaji wa kutoka Brazili ambaye amekuwa akifanya uuaji kwa muda mrefu sasa.

 

Pedro Redrigues Filho ni mmoja kati ya wauajiwa muda mrefu lakini yeye uuaji wake ulikuwa tofauti na wauwaji wengine Yeye alikua anaua wauaji na wahalifu tu. Anaelezewa kama mmoja wa wagonjwa wa akili (psychopath) na mchambuzi aliyekuwa anashughulikia kesi yake.

 

Amezaliwa katiko mji wa Minas Gerais mwaka 1954. Filho alikuwa na maisha yaliyogubikwa na mateso pamoja na vifo. Filho maisha yake ya unyanywasaji yalianza toka akiwa tumboni kwa mama yake ambapo baba yake alikuwa akimtesa sana mama yake japokuwa alikuwa na ujauzito, mateso yalipelekea Filho akapata  uharibifu (damage) kwenye fuvu la kichwa chake.

 

Kutokana na kukulia katika maisha yenye mateso, maumivu na matatizo mbalimbali Filho aliweza kujifunza jinsi ya kujieleza alipokuwa na miaka 14. Mtu wa kwanza kuuawa na Filho alikuwa mtu aliyemfukuza baba yake kazini. Baba yake na Filho alidaiwa (kusingiziwa) kuwa ameiba chakula hivyo Naibu meya wa jiji akamfukuza kazi kama adhabu ya wizi.

 

Filho alipopata habari hiyo alikasirika akachukua bastola akamuua meya mbele ya ukumbi wa jiji, lakini pia Filho hakuishia hapo alijua baba yake hakuwa mhalifu (mwizi) hivyo alianza kumtafuta mwizi aliyeiba chakula. Alipomkamata hakumpeleka kwenye vyombo vya dola bali alimuua.

Baada ya Filho kufanya tukio hilo ikabidi akimbie mji; alikimbilia eneo la Migi das Cruzes jijini Sao Paul, na akanguka penzini kwa mara ya kwanza. Lakini huko pia alifanya pia mauaji ya mtu aliyekuwa anajihusisha na madawa ya kulevya  na kuiba kwenye nyumba za watu.

Mpenzi wake huyo wa kwanza Maria Aparecida Olympia aliuawa na kikundi kimoja cha wahuni kipindi hiki  hajafikisha miaka 18.

 

Kifo cha mpenzi wake Olympia kilimfanya aamue kuwatesa na kuwaua watu wote walioshiriki kumuua mpenzi wake. Alilipiza kisasi cha mpenzi wake akiwa mwenyewe pekee, kabla ya kufikisha miaka 18 alipokuwa ashaua watu 10.

 

Filho alikuwa maarufu zaidi alipolipiza kisasi juu ya kifo cha mama yake mzazi. Na mlengwa alikuwa baba yake mwenyewe ambaye alimuua mama yake Filho kwa kumkatakata na mapanga.

 

IIikua hivi

Filho alimtembelea gerezani baba yake ambapo alimchoma na visu mara 22 kisha akachomoa moyo wa baba yake na kuutafuna.

 

Pia, siku moja alikuwa njiani ndani ya gari la polisi anasafirishwa akiwa na mtu mwingine ambaye alikuwa anatuhumiwa kwa makosa ya ubakaji, Filho alimuua mlemle ndani ya gari la polisi na polisi wakiwemo. Hapo ndipo alipoanza kuwa muuaji wa wauaji (The killer of killers).

 

Kaua wauaji 47 aliokuwa kafungwa nao gerezani. Moja kati ya mahojiano yake alisema “Thrill and joy out of killing other criminals” (furaha ya kuua wauaji).

 

Silaha yake aliyokuwa akiipenda kutekeleza mauaji ni upanga. Japo alifanya mauaji mengi, Filho aliachiwa huru, alikuwa amehukumiwa kifungo cha miaka 128 japokuwa sheria za Brazil haziruhusu mfungwa kufungwa zaidi ya miaka 30. Aliachiwa mwaka 2007 lakini aliahidi kuwaua waharifu wote nchini Brazil.

 

Leave A Reply