The House of Favourite Newspapers

IBADA ya Kuuaga Mwili wa Mama wa Mbunge Sugu, Muhimbili – Video

MWILI wa mama mzazi wa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu), Bi. Desderia Lungu Mbilinyi umeagwa leo Jumanne, Agosti 28, 2018 katika Kanisa Katoliki lililopo ndani ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili

Bi. Desderia Mbilinyi alifariki dunia juzi Jumapili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa kwenye wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) akipatiwa matibabu baada ya kuhamishwa kutoka wodi namba 18 kutokana na hali yake kuwa mbaya.

Viongozi Mbalimbali wa Serikali, vyama, dini, siasa, ndugu jamaa na marafiki wamejitokeza Muhimbili kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa mama Mbilinyi.

Miongoni mwa viongozi waliungana na familia na waombolezaji ni Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, baadhi ya wabunge ambao ni Halima Mdee wa Kawe, Ester Bulaya wa Bunda, na mtoto wa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, Fredy Lowassa na wengine.

Baada ya kuaga mwili wa marehemu utasafirishwa leo kwenda nyumbani kwake, jijini Mbeya kwa ajili ya maziko.

Na Edwin Lindege | Global Publishers

Comments are closed.