The House of Favourite Newspapers

IDFA Waendesha semina kwa waamuzi

0

 

Chama cha soka Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza  leo kimeendesha Semina ya mafunzo  maalumu kwa waamuzi watakaochezesha mashindano ya ligi ya taifa ngazi ya wilaya hiyo ambayo kwa mara ya kwanza itashirikisha wachezaji walioko chini ya miaka 20 kwa lengo la kukuza na kuendeleza soka na vipaji vya vijana hao kwa maslahi mapana ya taifa.

Mafunzo hayo ambayo yamefanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na kusimamiwa na mwamuzi mstaafu wa FIFA Alfred Lwiza ambaye amewataka waamuzi hao kuchezesha ligi hiyo ya Wilaya ya Ilemela kwa haki na kusimamia sheria zote 17 ” Ninawaomba waamuzi wachezesha ligi hii kwa kuzingatia sheria 17 za mpira wa miguu na kwakua TFF imeelekeza ligi zote za chini kuwa na vijana walioko chini ya miaka 20 muwasaidie kuzijua sheria kwakua wachezaji wengi wamezoea kucheza soka la mazoea” alisema

kwa upande wake Isarow Chacha ambaye ni mjumbe wa kamati ya waamuzi taifa (FRAT) amesema waamuzi waliopata fursa ya kushiriki semina hiyo wanatakiwa kutumia vyema ujuzi walioupata ili mkoa wa Mwanza uwe na waamuzi wengi wanaochezesha ligi mbalimbali hapa nchini ” Ukiangalia mkoa wa Mwanza hauna waamuzi wa kutosha wa kuchezesha ligi kuu na madaraja mengine  ila nyie mpo hivyo niwaombe kwamba mtumia ujuzi mlioupata hapa kuongeza juhudi ili nanyie mpate fursa ya kuchezesha mashindano makubwa hapa nchini kama ligi kuu nk” alisema

kwa upande wake Almas Mosh ambaye ni Katibu mkuu wa chama cha soka Ilemela amesema ligi  ya taifa ngazi ya wilaya hiyo inatarajiwa kuanza kuchezwa juni 18 mwaka huu ambapo jumla ya timu 8 zitashiriki ligi hiyo ” ligi yetu itaanza juni 18 na timu shiriki ziko nane mpaka sasa msimu huu tuna timu chache ambazo zitacheza ligi yetu hii ni kutokana na masharti ya TFF kututaka kucheza ligi hii kwa kutumia wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 hivyo tunaamini msimu ujao timu shiriki zitaongezeka na tamanio la TFF kuona soka likichezwa na vijana pekee litatimizwa” alisema

Leave A Reply