The House of Favourite Newspapers

Wananchi Magu walalamika kunyanyaswa na Muwekezaji, DC Atoa maelekezo.

0

Picha ni wananchi wakiwa katika mkutano na Mkuu wa Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza Rachel Kasanda kwa lengo la kueleza kero ya kunyanyaswa na muwekezaji wa kiwanda cha samaki Wilayani Magu.

UONGOZI wa Kijiji Cha Nyambilo Kata ya Nyangunge wilayani Magu mkoani Mwanza,umeiomba serikali kuingilia kati manyanyaso,Ukatili na Mauaji yanayosababishwa na muwekezaji wa Kiwanda Cha Samaki Tangreen Angriculture Limited kinachofanya shughuli zake wilayani humo.

Wakizungumza mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Magu Rachel Kasanda wananchi hao wameeleza kuwa Muwekezaji huyo amekuwa akikiuka makubaliano ya mipaka yake ndani ya ziwa Victoria kwa kusogeza vigingi (Bikoni) hali inayopelekea wavuvi wilayani humo kukosa eneo la kuvulia samaki na hali ya kimaisha kuwa mbaya zaidi kutokana na kutegemea ziwa hilo.

“Tunanyanyasika ziwa hili ni kama mgodi kwetu lakini kwa sasa ukienda kuvua samaki  walinzi wake wanakukamata wanakupeleka kwenye jumba la mateso,ukitoka salama unakuwa umelegezwa na hata ukienda kituo cha Polisi unakosa msaada, amesema Paul Charles Mkazi wa Nyambilo

Muwekezaji wa kutoka Tangreen Agriculture Limited Mr Chen akizungumza mbele ya mkuu wa wilaya ya Magu kwenye mkutano na wananchi uliofanyika wilayani humo hivi karibuni.

“Mhe, Mkuu wa Wilaya juzi tumemzika mdogo wangu baada ya kupigwa na walinzi wa muwekezaji wa kiwanda  hicho ambapo walimpiga na kusababisha majera makubwa yaliyopelekea kifo chake na pia Mzee mmoja jirani hapa tumemzika mara baada ya kipigo kikali kutoka kwa walinzi,na hakuna msaada wowote,”amesema Yohana Luhanga Mkazi wa Nyambilo.

Kwa upande wake Muwekezaji kutoka Tangreen Agriculture Limited Mr.Chen amesema amefanya hivyo kutokana na baadhi wa wananchi kutokuwa waaminifu na kubomoa Vizimba vyake na kuiba samaki.

“Kuna baadhi ya viongozi wa kiserikali na wananchi wanashirikiana kuvunja vizimba vyangu na kuiba samaki  mimi pamoja na serikali tunashindwa kufikia mafanikio tuliyojiwekea kutokana na baadhi ya viongozi kukosa uaminifu,”amesema Mr.Cheni.

Mkuu wa Wilaya ya Magu mkoani Mwanza Rachel Kasanda akizungumza mbele ya wananchi waliohudhuria mkutano huo uliokua na lengo la kueleza kero na manyanyazo wanayopata kutoka kwa Muwekezaji wa Tangreen Agriculture Limited.

Mkuu wa Wilaya ya Magu Rachel Kasanda amesema amesikiliza pande zote mbili na kuwataka maafisa Uvuvi pamoja na mwekezaji kwenda kunyoosha mipaka upya ili eneo la kuvua samaki wananchi libaki wazi na wananchi wasiingilie eneo la Muwekezaji.

 

Leave A Reply