The House of Favourite Newspapers

Iggy Azalea adunda mtaani na pete aliyovalishwa na Nick Young

0

nick-young-600x800Nick Young na Iggy Azalea

CALIFORNIA, Marekani

LICHA ya kusalitiwa, rapa wa kike, Iggy Azalea ameonekana akiwa na pete ya uchumba aliyovishwa na mpenzi wake, Nick Young ambaye ni staa wa NBA, hii inamaana kuwa wapo poa na wanaendelea vyema kwenye penzi lao.

Hivi karibuni, Nick Young anayechezea timu ya Los Angeles Lakers, akiwa anavaa jezi namba sifuri, alirekodiwa na mchezaji mwenzake akisimulia wenzake kuhusu uhusiano na wanawake wengine na ‘clip’ hiyo inadaiwa ilimfikia Iggy ambaye ilihofiwa kuwa angemuacha.

Rasmi Iggy Azalea, 25, amesema yeye na Nick Young, 30, wataishi pamoja licha ya kuwa na taarifa za kumsaliti lakini hilo hajali kwa kuwa hana uthibitisho, hivyo hawezi kuamini maneno ya watu kuhusu usaliti uliofanywa na Nick Young.
Iggy Azalea Ijumaa iliyopita alionekana akiwa na pete hiyo ya dhahabu yenye thamani ya dola 500,000 (zaidi ya Sh bil moja) aliyoiachia wazi na kuonekana kama mtu aliyekuwa akitaka watu waone kuwa ameivaa, kwenye mitaa ya Beverly Hills, California ambako alikwenda kufanya ‘shopping’.

Mapema wiki iliyopita Iggy Azalea aliandika kwenye Twitter: “Sijawahi kuachana na Nick. Tupo pamoja. Muda wote nawajibu maswali yenu vizuri lakini kazi yangu ni kuutangaza muziki wangu na siyo uhusiano wangu.”

Leave A Reply