The House of Favourite Newspapers

IGP SIRO AFIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU AKWILINA KUTOA POLE KWA FAMILIA

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni (kushoto) akizungumza jambo na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Nyakoro Sirro, leo kwenye msiba wa aliyekuwa  mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini, Mbezi Jijini Dar, Akwilini aliuawa kwa kupigwa risasi Ijumaa ya juzi  eneo la Mkwajuni, Kinondoni, Dar.
Wanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji (NIT) wakiwa msibani.
Dada wa marehemu, Segolena Uwiso (katikati) ambaye ndiye aliyemlea tangu akiwa na miaka miwili akilia.
Rafiki wa karibu wa marehemu akilia kwa uchungu akiwa msibani.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Nyakoro Sirro akizungumza jambo na wanafamilia msibani.
Rais wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mchinja Usman (kulia) akiongea na wanafunzi wa chuo chake msibani.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Nyakoro Sirro, leo amefika kwenye msiba wa aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi juzi Ijumaa eneo la Mkwajuni, Kinondoni, Dar. Msiba huo upo nyumbani kwao Akwilina maneo ya Mbezi jijini Dar.

(PICHA: RICHARD BUKOS | GLOBAL PUBLISHERS)

Comments are closed.