The House of Favourite Newspapers

IGP SIRRO AKUTANA NA IGP WA SUDAN

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro,  leo Agosti 30, 2019,  amekutana na Mkuu wa Jeshi la Polisi la Sudan, IGP Adil Mohamed Ahmed jijini Dar es Salaam.

IGP Ahmed yuko nchini hapa kwa ziara  ya kikazi ya siku mbili  ya kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya majeshi ya polisi ya  Tanzania na Sudan.

 

Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Sudan, Adil Mohamed Ahmed (kushoto), akisaini kwenye kitabu cha wageni alipowasili makao makuu ya Jeshi la Polisi nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili iliyolenga kuimarisha ushirikiano uliopo kati majeshi ya polisi ya Tanzania na Sudan.   
IGP Ahmed  akizungumza na  makamishna na maofisa wakuu waandamizi wa jeshi la polisi nchini (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam.
…Akimpa zawadi IGP Sirro.
IGP Ahmed na IGP  Sirro wakiwa na  makamishna na maofisa wakuu waandamizi baada ya kumaliza kikao kilichofanyika makao makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam.

(Picha: Na Jeshi la Polisi Nchini)

 

Comments are closed.