The House of Favourite Newspapers

Sirro: Walizani Hamza ni Mtu wa Kawaida, Tumeapa Kufa kwa Risasi – Video

0

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Nyakoro Sirro amesema tukio la mauaji ya askari wanne lililotokea juzi jijini dar es Salaam ni tukio kubwa kwa Jeshi la Polisi lakini ndio kazi ya askari, na sasa wamepata kitu cha kujifunza kama askari, wananchi wao wana kitu cha kujifunza na wafiwa nao wana kitu cha kujifunza.

 

Sirro amesema hayo wakati wa kuaga miili ya askari hao jijini Dar es Salaam; “Ukishakuwa na mtoto mhalifu, mwizi, gaidi au mwenye tabia mbaya mbaya usiposhirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kuna mawili; anaweza akaleta madhara kwa Watanzania ama uhai wake ukapotea.

 

“Huyu Hamza aliyoyafanya kama ndugu zake wangewajibika vizuri leo tusingekuwa hapa ndani, lakini Watanzania wajue kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vipo kwa ajili ya kulinda usalama wa Watanzania, ndio maana tumeapa kwa Amri Jeshi Mkuu kufa kwa risasi, hatuoni tabu.

 

“Lazima Watanzania wajue kwamba na sisi tuna familia zetu, ukishajua kwenye familia yako kuna mhalifu ujue wewe ni tatizo kwa Watanzania, tunategemea uzae mtoto ambaye kesho atakuwa Waziri, IGP au mwalimu, lakini ukizaa mtoto akawa mwizi, paruanja ni tatizo.

 

“Kwa wafiwa kuna kitu cha kujifunza, askari wetu hawakuwa magaidi, hawakuwa wezi, hawakuwa majambazi, wamekufa wakilinda Watanzania, kifo chao ni kwa heshima ya Watanzania, tusipate huzuni sana, tuwaombee kwa sababu walichokuwa wanafanya ni ajili ya kuwatetea Watanzania.

 

“Kwa police officers na viongozi wa ulinzi na usalama kutokana na wenzetu kufa kwa kupigwa risasi vichwani, huwa nawaambia siku zote usicheze na mtu wa hovyo hovyo, usimwamini kila mtu, hii ni kwa sababu ya imani.

 

“Waliopomuona huyu mtu wa hovyo hovyo Hamza akiwasogelea walijua ni Mtanzania wa kawaida, kumbe alikuwa na bastola na akafanya alichofanya, ni kitu tumejifunza, ukizubaa usilaumu jeshi, usilumu serikali, askari mna mafunzo ya kutosha, sio kila mtu ni rafiki.

 

“Tumepoteza vijana wadogo sana, sisi tunaokaribia kustaafu tunajua hawa ndio wangekuja kuliendesha jeshi hapo baadae, lakini kwa sababu ni sehemu ya maisha yetu. Mliobaki mmejifunza, sio kila mtu anapenda askari polisi au vyombo vya dola.

 

“Wakati mwingine tunaambiwa tunatumia nguvu kubwa sana au hatutendi haki sio? Lakini yanapotokea hapa sisikii mtu anazungumzia haki ya polisi, kusiwe na double standard, kazi hii ni ngumu sana, mtu akiona hivi anazani ni rahisi, kushughulika na mhalifu sio jambo dogo.

 

“Tuwaombee sana, wametangulia mbele ya haki na sisi tupo nyuma yao, mliofiwa si kwamba mmefiwa nyie tu, na sisi tumefiwa kwa sababu walikuwa vijana wetu, sisi tunaovaa buti bila kujali mgambo au nani huwa nasema sote ni kitu kimoja, tunalinda amani.

 

“Niwahakikishie ndugu wa marehemu kwamba, tutajihadi kwa mujibu wa kanuni zetu, vijana wetu hawa wanapata haki zao kama wana familia zao, watapata haki zao, niwashukuru sana, asanteni, asanteni sana,” amesema IGP Sirro.

Leave A Reply