The House of Favourite Newspapers

IGP Sirro: Wazazi Wengine Wasituzalie Watoto Kama Hamza – Video

0

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Nyakoro Sirro amesema kuwa ndugu wa Hamza Hassan Mohammed aliyeua askari wanne kabla ya yeye kuuawa na polisi wanaweza kwenda kuchukua mwili wa ndugu yao kwa kuwa wameshamaliza kuufanyia kazi.

 

Hamza aliuwawa Agosti 25, 2021 kwa kupigwa risasi na polisi dakika chache baada ya kuwauwa askari polisi watatu na mlinzi wa kampuni binafsi karibu na ubalozi wa Ufaransa na daraja la Salenda jijini Dar es Salaam.

 

IGP Sirro ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Agosti 28, 2021 wakati Jeshi la Polisi likiwaaga Makamishna wake, Balozi Valentino Mlowola na Robert Boaz amesema kuwa tayari wameshaufanyia kazi mwili huo hivyo ndugu zake wanaweza kwenda kuuchukua na wakishindwa mwili huo utazikwa na Halmashauri.

 

Sirro amesema iwapo ndugu watachelewa basi mwili huo unaweza kuzikwa na manispaa huku akiwaasa wazazi kutokuzaa watoto wenye tabia kama alizokuwa nazo Hamza.

“Hiyo familia ya Hamza [Mohammed] inajisikiaje? Fikiria wewe ungekuwa baba yake Hamza, mama yake Hamza, mdogo wake, ungejisikiaje kuzaa kwako umetuletea balaa Watanzania. Kwa hiyo naomba Watanzania wengine wasituzalie watoto kama Hamza.”- IGP Simon Sirro

TAZAMA VIDEO SIRRO AKIZUNGUMZA

Leave A Reply