The House of Favourite Newspapers

Ijue Saratani ya Shingo ya Kizazi na Namna ya Kujikinga

HII ni saratani inayojitokeza katika shingo ya kizazi na kusambaa ndani na nje ya kizazi. Hii ni kutokana na ukuaji usio wa kawaida wa chembe hai sehemu hiyo. Seli au chembe hai hizi zina tabia ya kusambaa kwa kasi na kushambulia maeneo mengine ya mwili. 

 

Tatizo linapotokea huwa hakuna dalili kubwa za awali zaidi ya kutokwa na damu ukeni, maumivu ya nyonga na maumivu wakati wa tendo la ndoa, wakati mwingine damu inatoka baada ya tendo la ndoa.

 

Vijidudu vinavyosababisha ugonjwa huu ni virusi viitwavyo Human Papilloma Virus (HPV) ambavyo vimeonekana kwa zaidi ya asilimia 90. Mtu ambaye alishawahi kupata maambukizi haya awali na akapona, hawezi kupata tena kwa kuwa tayari anakuwa ameshatengeneza kinga ya kudumu dhidi ya vijidudu hivi vya HPV.

 

JINSI TATIZO LINAVYOTOKEA

Saratani huanzia pale mtu anapopata chanzo yaani Virusi vya HPV hadi ugonjwa kujitokeza kabisa huchukua kati ya miaka kumi hadi ishirini na mambo yanayochangia kujitokeza au kupata saratani ni uvutaji wa sigara, udhaifu wa kinga mwilini, kuanza ngono katika umri mdogo mara tu baada ya kuvunja ungo au kabla ya hapo na kuwa na wapenzi wengi au kubadilisha wapenzi unaofanya nao ngono mara kwa mara.

 

Aina ya saratani ya shingo ya kizazi inayojitokeza zaidi inaitwa Squamous Cell Carcinoma ingawa ipo nyingine iitwayo Adenocarcinoma.

DALILI ZA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

Katika hatua za awali, saratani ya shingo ya kizazi huwa haioneshi dalili zozote. Dalili huanza kujitokeza baadaye sana, mfano kutokwa na damu ukeni bila mpangilio kama vile baada ya damu ya hedhi au kwa mama aliyekoma hedhi halafu anaanza ku-bleed ukeni, kutokwa na damu ukeni pale unapojisafisha au wakati wa kufanya tendo la ndoa hasa baada ya kumaliza.

 

Katika hali ya kawaida, mwanamke mwenye saratani ya shingo ya kizazi huwa hana uvimbe ukeni. Wakati mwingine unapata maumivu unapofanya tendo la ndoa pamoja na kutokwa na damu bila ya mpangilio. Mwanamke mwenye tatizo hili vilevile huweza kutokwa na majimaji ukeni yenye harufu mbaya, lakini hakuna muwasho.

 

Saratani ya shingo ya kizazi ikichelewa kugundulika na kutibiwa husambaa hadi tumboni, kwenye mapafu na sehemu nyingine za mwili na kusababisha dalili kama kukosa hamu ya kula, kupungua uzito, maumivu ya kiuno, mgongo na miguu, miguu kuvimba, kutokwa na damu nyingi nzito, mifupa kuvunjika yenyewe, mkojo na choo kikubwa kutoka bila mpangilio.

 

UCHUNGUZI

Saratani ya shingo ya kizazi huchunguzwa hospitalini. Inashauriwa mwanamke yeyote aliye katika umri wa kuzaa awe na tabia ya kupima mara kwa mara hospitalini. Saratani ya shingo ya kizazi, upimaji wa mapema ni muhimu kujua kama mabadiliko yameanza. Kama tayari, basi utapata tiba kabla tatizo halijawa kubwa. Vipimo vinavyotumika kupima saratani ni Pap Smear ingawa vipimo vingine ni Ultrasound na X-Ray, vipimo vya damu, mkojo pia vitatumika.

TIBA NA USHAURI

Saratani ya shingo ya kizazi ina hatua nne kuu na ikigundulika mapema hutibiwa na kupona kabisa hasa katika hatua za kwanza na ya pili kidogo. Matibabu mengine hutegemea na hatua ambazo ugonjwa umefikia kwa hiyo kuna kupata nafuu au kutopona kabisa kwa hiyo ni vema kuwa na utaratibu wa kufanya uchunguzi mara kwa mara katika vituo vya afya na hospitali za wilaya.

 

Kinga ya saratani ya shingo ya kizazi ni kujiepusha na ngono katika umri mdogo, kuepuka kuwa na wapenzi wengi au kubadilishabadilisha wanaume unaofanya nao ngono.

 

Hakikisha unaye mpenzi mmoja unayemwamini na epuka ngono zembe. Jiweke katika hali ya usafi hasa katika sehemu za siri na kuepuka maambukizi ya mara kwa mara ukeni ikiwa yatajitokeza, tibu

Comments are closed.