The House of Favourite Newspapers

Ijue siri ya boga kwenye urembo wa ngozi!


black-women-wedding-makeup-picturesB
oga ni tunda zuri ambalo lina mbegu, linaweza kuifanya ngozi yako kuvutia na kuwa nyororo kama utalitumia kwa ufasaha kwani lina Vitamini C ya kutosha kabisa na Caroteniods ambayo unaweza kuipata kwenye mboga ya karoti.

43737-boga2b1.jpgBoga linao uwezo wa kutibu kidonda kwenye ngozi yako.

Kama unataka kutengeneza maski kwa ajili ya uso wako ili kuikomboa ngozi yako unaweza ukafuata njia hizi;

Chukua kipande 1 kidogo cha boga, changanya na ΒΌ kikombe cha maziwa

166_health-beauty-antalyaMaandalizi.

Ondoa ngozi ya boga na mbegu zake, kisha likatekate na uweke kwenye chombo.

Baada ya hapo, weka jikoni ulipike mpaka lilainike.

Chukua vijiko viwili vya maziwa uchanganye kwenye boga lako kisha ongeza robo kikombe cha maji kisha changanya mpaka upate mchanganyiko mmoja.

Ukishachanganya hakikisha unapaka uso wako, kama ni usiku lala kisha osha asubuhi kwa maji ya vuguvugu.

Comments are closed.