The House of Favourite Newspapers

Yamoto Band kuachia mpya Des. 19 Dar Live

YAMOTO.pngMusa Mateja

BAADA ya kubamba na Ngoma ya Cheza kwa Madoido, bendi inayotikisa kila kona, Yamoto inatarajia kushusha ngoma mpya ijulikanayo kama Imo, Desemba 19 ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live.

Akizungumza na Showbiz, mratibu wa shoo hiyo, Mohamed Seif ‘Mudy K’ alisema kuwa mbali na utambulisho wa ngoma hiyo, pia kutakuwa na sapraiz kibao za Kibongo Fleva sambamba na kumtambulisha Baby J kutoka Zanzibar na Kayumba (mshindi wa BSS 2015).

“Hii si ya kukosa kwani usiku huo familia yote ya Mkubwa na Wanawe itahamia Dar Live ambapo kiingilio kitakuwa shilingi 10,000,” alisema Mudy K.

Comments are closed.