The House of Favourite Newspapers

Imevuja! Demu wa Marekani wa Nay alikuwa wa Ivan

0

stella tillyaStella Tilya ‘Chaga Baby’

Na Musa Mateja
IMEVUJA! Wakati kumbukumbu bado zinaonesha maumivu makubwa aliyokuwa anayapata mume wa Zari, Ivan Semwaga kwa mkewe kuchukuliwa na Diamond Platnumz, imethibitika kuwa mpenzi wa sasa wa Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ Stella Tilya ‘Chaga Baby’ ambaye anaishi Marekani ni ‘mzigo’ wake.

nay (2)Nay wa Mitego

Mganda huyo mwenye makazi yake nchini Afrika Kusini, hivi karibuni alimcharukia Nay akimtaka kuachana na Stella.

Ishu hiyo imevuja siku chache baada ya Nay kuweka wazi uhusiano huo na Chaga Baby huku wakijiachia kwa raha zao katika mitandao mbalimbali ya kijamii, jambo ambalo limemkera Ivan na kujikuta akimpiga mkwara mpenziwe huyo aliyelazimika kumjulisha Mbongo Fleva huyo kinachoendelea.

ivan-SSEMWANGAIvan Semwaga

Inadaiwa na chanzo chetu kuwa Chaga Baby alikuwa ni mpenzi wa muda mrefu wa Ivan tangu alivyoachana na Zarinah Hassani ‘Zari’. Awali wasichana hao wawili walikuwa ni marafiki na inadhaniwa mumewe Zari alifanya hivyo makusudi ili kumkomoa mwenzake aliyeamua kuzaa na Diamond.

“Kama ungekuwa unafuatilia mitandao ya Uganda ungekuwa umeona jinsi magazeti ya nchi hiyo yalivyomponda Ivan, yakimwambia kwa nini amekuwa akiporwa mademu zake na wasanii wa Kibongo huku akiwa na fedha ya kuweza kufanya jambo lolote, yaani wanamwambia hivyo kwa kuwa walikuwa wakijua wazi Chaga Baby ndiye amekuwa akimnadi kama mbadala wa Zari,” kilisema chanzo hicho.

Gazeti hili lilithibitishiwa na Nay wa Mitego juu ya mpenzi wake kupigwa mkwara na Ivan na kwamba amemuonesha hata baadhi ya meseji alizokuwa akimtumia, akimlaumu kwa kumsaliti.

“Huyu jamaa mimi namuona kama anatangatanga maana hajui uhusiano wetu ulianza lini, kweli nimeona meseji zake akinichimbia mkwara, ninachoweza kusema kwa sasa si mtu wa kubabaishwa kwa lolote lile maana siku zote nimekuwa nikisimamia uamuzi wangu,” alisema.

Leave A Reply