visa

INASIKITISHA MTOTO AUAWA, ATUPWA KWENYE KARO LA CHOO

VITENDO vya utekaji na mauaji ya watoto vinavyoendelea katika Manispaa ya Lindi, vinazidi kuwapa wakati mgumu wananchi wa mkoa huo baada ya mtoto mwingine Husseni Fadhili (7) mkazi wa Mitaa ya Benki, kudaiwa kuuawa na watu wasiojulikana na mwili wake kutupwa kwenye karo la choo.

 

Tukio hilo la kusikitisha lililoacha maswali mengi limeibua mshangao mkubwa miongoni mwa jamii, baada ya Husseni aliyekuwa anasoma darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Msinjahili, Manispaa ya Lindi kutoweka kitatanishi nyumbani kwao kisha kukutwa amekufa ndani ya karo la choo cha Kituo cha Mabasi Lindi Mjini, Juni 11 mwaka huu, saa 12:00 asubuhi.

 

Hili ni tukio la pili ndani ya kipindi cha miezi miwili mtoto kukutwa akiwa amefariki dunia baada ya kutoweka nyumbani kwao ambapo Aprili 9 mwaka huu, mtoto Mutifati Abdallah (5) aliyekuwa anasoma chekechea katika Kanisa la Assembles of God mjini Lindi kuchukuliwa kwa njia zinazodaiwa za kishirikina na mwili wake kukutwa umetelekezwa kando ya Bahari ya Hindi, Aprili 14 mwaka huu, huku ngozi, macho na ubongo vikitolewa na wauaji.

 

Zena Hamisi Mjoka (34), mama mzazi wa mtoto Husseni Fadhili akizungumza hivi karibuni na mwandishi wa habari hii nyumbani kwake Mtaa wa Benki, alisema kijana wake alitoweka kitatanishi Jumapili ya Juni 9 mwaka huu, saa 11:30 za alasiri na kuonekana siku ya Jumanne ya Juni 11 mwaka huu saa 12:00 asubuhi akiwa mfu huku mwili wake ukiwa umetoswa ndani ya karo la choo.

 

Baadhi ya mashuhuda wa mwili wa mtoto Husseni akiwemo mama lishe aliyejitambulisha kwa jina moja la Nganje na wale waliousindikiza mwili wake Hospitali ya Mkoa ya Sokoine kuufanyia uchunguzi, wamedai nyeti, ngozi maeneo ya mikononi, miguuni na tumboni zimeondolewa.

Hata hivyo, Zena alikuwa na haya ya kusema: “Huwa nashinda Kituo cha Mabasi Lindi nauza korosho zilizobanguliwa na siku hiyo Husseni alinifuata nikampatia chakula na kumruhusu arejea nyumbani na mimi kuendelea na biashara yangu, alikwenda nyumbani,” alisema Zena huku akilengwalengwa na machozi.

 

Aliongeza kuwa aliporejea nyumbani kwake saa 2:00 usiku, hakuweza kumkuta mwanaye hivyo kuzua taharuki kwa upande wake na kuanza kumtafuta maeneo mbalimbali, hata kwa majirani, ndugu, jamaa na viwanja vya michezo, bila mafanikio.

 

Alisema baada ya maeneo yote hayo kumtafuta bila mafanikio, alitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Benki, Zuhura Shaziri na baadaye polisi Kituo cha Lindi Mjini ambapo walimpatia RB.

 

Alisema baadaye alipata taarifa kwamba kuna karo amekutwa mtoto akiwa ametupwa humo na Mtoto auawa, atupwa karoni! alipokaguliwa ilijulikana kuwa ni wake. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, ACP Pudensiana Protas amethibitisha kuokotwa kwa mwili wa mwanafunzi Husseni ndani ya karo la choo.

 

“Nawaomba wafiwa wawe na utulivu kipindi hiki cha majonzi na serikali kupitia Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo,” alisema kamanda huyo.

 

Gazeti hili linatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa mtoto Husseni na linaomba jeshi la polisi liharakishe uchunguzi wa tukio hilo ili kama kuna waliohusika waweze kupatikana na hatua za kisheria zichukuliwe

 

na kuanza kumtafutamaeneo mbalimbali, hatakwa majirani, ndugu, jamaana viwanja vya michezo, bilamafanikio.Alisema baada ya maeneoyote hayo kumtafuta bilamafanikio, alitoa taarifa kwaMwenyekiti wa Mtaa wa Benki,Zuhura Shaziri na baadayepolisi Kituo cha Lindi Mjiniambapo walimpatia RB.

 

Alisema baadaye alipatataarifa kwamba kuna karoamekutwa mtoto akiwaametupwa humo na alipokaguliwa ilijulikanakuwa ni wake.

 

Kamanda wa Polisi Mkoawa Lindi, ACP Pudensiana Protas amethibitishakuokotwa kwa mwili wamwanafunzi Husseni ndaniya karo la choo.“Nawaomba wafiwawawe na utulivu kipindi hiki cha majonzi naserikali kupitia Jeshi laPolisi linaendelea nauchunguzi kuhusu tukiohilo,” alisema kamandahuyo.

 

Gazeti hili linatoapole kwa ndugu, jamaana marafiki wa mtotoHusseni na linaombajeshi la polisi liharakisheuchunguzi wa tukiohilo ili kama kunawaliohusika wawezekupatikana na hatua zakisheria zichukuliwe.
Toa comment