The House of Favourite Newspapers

Inatisha! Mafuriko Yaua Watu 194 Kenya

0

MVUA  kubwa zilizonyesha nchini Kenya zimeua watu 30 hivi karibuni na kufanya idadi ya jumla ya watu 194 kupoteza maisha ndani ya mwezi mmoja, huku wengine zaidi ya 122,000 wakiyapoteza makazi yao ndani ya kipindi hichohicho cha mwezi mmoja kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua hizo kubwa.

 

Mamlaka nchini Kenya zimewataka watu wanaoishi katika maeneo yanayokumbwa na mafuriko, kama vile kando ya mito, kuondoka haraka katika maeneo hayo kwani hali inazidi kuwa mbaya na huenda yakatokea maafa makubwa zaidi kwani mvua kubwa zaidi zinatarajiwa kunyesha mwezi Juni mwaka huu.

 

Gazeti la Daily Nation limemnukuu Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Fred Matiangi akisema kwamba viongozi wako tayari kuwatoa “kwa nguvu” watu walio katika hatari.

 

“Hatuna chaguo jingine. Tutahamisha watu kwa nguvu, hata ikiwa tutawasafirisha wenyewe kwa malori, tutafanya hivyo, afisa mmoja ameliambia Gazeti la kila siku la Standard Digital.

 

Kwa wale ambao hawajui wapi pa kwenda, mamlaka imetenga shule zilizofungwa kwa sababu ya marufuku ya watu kutotembea kutokana na janga la Corona. Shule hizi zitatumiwa kama hifadhi kwa muda kwa familia zilizohamishwa.

 

Mamlaka pia inasema serikali itatoa msaada wa chakula, maji na fedha kupitia simu kwa familia zilizohamishwa.

 

Leave A Reply