Infinix Zero 8; 64+48 Kamera Yazinduliwa Tanzania

Mara baada ya tetesi za muda mrefu juu ya ujio wa Infinix ZERO 8, hatimaye kampuni ya simu ya Infinix kupitia mitandao yake ya kijamii @infinixmobiletz wameitambulisha rasmi Infinix ZERO 8. Kwa mujibu wa kampuni ya Infinix, Infinix ZERO ndio kinara ‘flagship model’ kwa mwaka huu wa 2020 na ikiwa kama simu yenye kuiwakilisha kampuni ya Infinix, Infinix ZERO 8 imebeba sifa lukuki kama zifuatazo;

MTK Helio G90T processor na RAM ya GB 8+ 128 ROM, vinaifaya Infinix ZERO 8 kuwa na ufanisi zaidi wa kufungua /kubeba videos na games zenye ukubwa wa aina yoyote pasipo kugoma goma. Vile vile Infinix ZERO 8 ina teknolojia ya 3D hii ni maalumu kwajili ya kupunguza joto endapo utaitumia simu yako kwa muda mrefu. Infinix ZERO 8 ina kamera zenye kubeba megapixel kubwa, nyuma ikiwa ni 64 mbele 48 na IMX686 Sensor maalumu kwajili ya picha kali na zenye uhalisia pasipo kujali muda wala mazigira.

Infinix ZERO 8 inauwezo wa kudumu na chaji kwa zaidi ya siku moja kutokana na ujazo wake wa mAh 4500 na 33W Super change yenye battery kwa dakika chache. Muonekano wa Infinix ZERO 8 ni wakitajiri, naweza sema ina design yenye kuvutia kutokana na umbo lake kuwa jembamba lenye kutawaliwa na wigo mpana wa kioo cha inch 6.85FHD+.

Kwa sasa Infinix ZERO 8 ipo Tanzania na unaweza kuipata katika maduka yote ya simu kwa bei isiyozidi Tsh.750,000/=
Toa comment