The House of Favourite Newspapers

INIESTA ATANGAZA KUSEPA BARCELONA

UHISPANIA: Kiungo mchezeshaji wa klabu ya Soka ya Barcelona, Andres Iniesta (33) ametangaza kuondoka klabuni hapo ifikapo mwisho wa msimu huu 2017/18.

Kiungo huyo raia wa Uhispania aliyeichezea klabu hiyo kwa miaka 22 na kushinda mataji 31 amesema hataweza kucheza dhidi ya Barcelona atakapoondoka klabuni hapo.



Iniesta maarufu kama ‘Magician’ ni mchezaji pekee kuwahi kuwa mchezaji bora (Man of the match) katika fainali ya EUROs, fainali ya Kombe la Dunia na fainali ya Klabu Bingwa Ulaya
.

Kiuongo huyo bora duniani anatarajiwa kwenda kukipiga China ambapo inadaiwa atalipwa mkwanja mara mbili ya ule anaolipwa Barcelona. Aidha, Iniesta amesema hataki tena kucheza Soka Bara la Ulaya kwa sababu atakutana katika mechi na timu yake iliyomlea Barcelona jambo ambalo anaona kwake haitakuwa vyema kupambana na mlezi wake.

Comments are closed.