The House of Favourite Newspapers

IMEBAINIKA! SABABU YA KIBA KUMPA DIAMOND ‘NGUMI’ HII HAPA

Nasibu Abdul ‘Diamond’ Akisalimiana na Ali Saleh Kiba ‘AliKiba’

DAR ES SALAAM: MAMBO ni moto! Licha ya hivi karibuni staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kujishusha na kumsalimia kiroho safi staa mwenzake, Ali Saleh Kiba ‘AliKiba’ pale walipokutana kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar kuuaga mwili wa Video Queen Agness Gerald ‘Masogange’, habari mpya ni kwamba Kiba amezidi kulikoleza bifu lao lililodumu kwa muda mrefu, Amani linakupa habari kamili.

 

Uchunguzi wa gazeti hili uligundua kwamba, licha ya Diamond kumpa salamu kwa kumnyooshea mkono, Kiba alimgeuzia kiganja (mkono akiwa ameukunja mithiri ya ‘ngumi’), akabaki amekaa bila kusimama kama walivyofanya wengine, hali iliyozua gumzo mitandaoni na watu kujiuliza kwa nini msanii huyo aliamua kumfanyia mwenzake hivyo.

“Kiukweli Kiba alionesha tabia ya ajabu pale Leaders, huenda ana sababu zake lakini sijui kwa nini amekuwa na moyo wa aina hii,” alisikika akisema mmoja wa wadau waliokuwa eneo hilo.

 

 

KIBA AKOLEZA BIFU

Katika kile kilichoonekana ni kulikoleza bifu lao, Kiba amemtosa mazima msanii mwenzake huyo kwa kutompa mwaliko wa sherehe ya harusi yake inayotarajiwa kufanyika kesho Aprili 29, katika Hoteli ya Serena jijini Dar ikiwa ni baada ya kufunga ndoa huko Mombasa-Kenya.

 

“Kiba anaonekana bado hayuko poa na Diamond, kamfanyia mwenzake jambo la kushangaza sana maana huwezi amini hadi dakika hii (Jumatatu) hajamualika kwenye sherehe yake ya harusi, yaani inaonekana Kiba hayuko tayari kushirikiana na mwenzake maana mara nyingi amekuwa akijishusha lakini hampi ushirikiano,” kilidai chanzo kilicho karibu na Kiba.

 

KIBA ANASEMAJE?

Amani lilijaribu kumvutia waya Kiba lakini simu yake ya mkononi iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.

MENEJA APOKEA

Alipotafutwa meneja wa Kiba anayejulikana kwa jina la Aidan Seif juzi na kuulizwa kama wamemualika Diamond katika harusi hiyo au wamempiga pini, alijibu kwa kifupi na kuomba asiongelee kwa undani suala hilo.“Hadi sasa hatujamualika na kwa kweli sijajua kama tutamualika,” alisema Aidan.

 

SIRI YA SALAMU YAO SASA…

Kufuatia hivi karibuni kukutana na Diamond kumpa mkono Kiba lakini akamgeuzia kiganja, mengi yamekuwa yakisemwa, baadhi wakidai ni staili tu kama zilivyo staili nyingine za kupeana mikono lakini wengine wakahusisha salamu ile na mambo ya kinyota.

“Unajua hii ya Kiba kugeuza kiganja inaweza kuwa na tafsiri yake, moja waislam wengi huwa wanafanya hivyo lakini niliwahi kusikia pia kuwa, kama una nyota inayong’ara, mtu akisalimiana na wewe, kama kaelekezwa na mtaalam jinsi ya kuichukua nyota yako, akigusanisha mkono na wewe, anaweza kuichukua, huenda Kiba alifanya vile kulinda nyota yake,” alidai Jafari wa Magomeni jijini Dar.

 

MSIKIE MTAALAM HUYU

Mmoja wa wataalam wa masuala ya nyota ambaye amekuwa akitoa elimu mtandaoni aliyefahamika kwa jina la Sued Kessy aliwahi kusema kuwa, kuna uhusiano mkubwa kati ya kiganja na nyota ya mtu.

“Mimi niseme tu kwamba, kiganja na mambo ya nyota vina ukaribu sana, ukiangalia sehemu ya mbele ya kiganja kuna mistarimistari ambayo kila mmoja una maana yake, kwa mfano kuna wa afya, fedha, ndoa, mafanikio na kadhalika. “Hivyo alichokifanya Kiba huenda ilikuwa ni salamu ya kawaida tu lakini nikuambie tu kwamba, yawezekana pia alifanya vile kulinda nyota yake,” alisema mtaalam huyo.

 

DIAMOND ANAJISHUSHA SANA…

Licha ya kwamba mastaa hao wana bifu lakini Diamond amekuwa akijishusha mara nyingi kwani hata hivi karibuni alimtakia heri ya kufunga ndoa pia katika TV yake ya Wasafi iliyofunguliwa hivi karibuni imekuwa ikipiga nyimbo za Kiba.

 

BI SANDRA NAYE…

Siyo Diamond tu, hata mama yake mzazi, Sanura Kassim ‘Sandra’ kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram alimtakia Kiba heri ya ndoa lakini aliambulia matusi ya nguoni kutoka kwa mashabiki wa Kiba yaani Team Kiba.

 

TUJIKUMBUSHE

Kwa kipindi kirefu Diamond na Kiba wamekuwa mahasimu ambapo Jumapili iliyopita walikutana katika shughuli ya kuuaga mwili wa Masogange iliyofanyika katika Viwanja vya Leaders na kusafirishwa kwenda jijini Mbeya ambako mazishi yalifanyika Jumatatu.

Stori: Mwandishi Wetu, Amani

Comments are closed.