The House of Favourite Newspapers

Irene Uwoya Jifunze Uzuri Una Mwisho

0

UNAPOKUWA na pesa ni vigumu sana na nidhamu. Pesa zinaleta kiburi, majivuno na usipoangalia pesa hizo hizo zinaweza kukuua.

Muigizaji Irene Uwoya kwa sasa anaonekana kutembelewa na fedha.

 

Bahati mbaya sana fedha hizo hazijulikani zinatokana na kazi gani anayoifanya lakini itoshe kusema kwamba bibie fedha za kufanya kufuru anazo.Kwa tunaomfuatilia kwenye mitandao yake ya kijamii pamoja na vyombo vya habari, hakika ni mashahidi wa mambo mengi yanayoashiria kwamba anazitumbua fedha.

 

Kama umesahau, nikukumbushe tu ndiye aliyefanya kufuru juzikati wakati mtoto wake alipopata Komunio ya Kwanza.Watu mbalimbali walialikwa, walikula na kunywa vibaya sana.

Kama hiyo haitoshi, kuna wakati wa kutunza ulifika, alimwagia mapesa kama yote mama yake mzazi. Ilikuwa ni kufuru kwelikweli. Watu walipigwa na butwaa siku hiyo.Baada ya siku chache kupita, taarifa zinaeleza kwamba yeye pamoja na kamati yake ya sherehe hiyo walikwea pipa kuelekea visiwani Zanzibar kwenda kuvunja kamati.

 

Unaambiwa huko nako alikwenda kutumia pesa ili imzoee.Usisahau Uwoya huyuhuyu aliwahi kufanya bonge la bati linalodaiwa kuteketeza mapesa mengi kwenye boti. Walikuwa wakisherehekea siku yake ya kuzaliwa. Uwoya huyu huyu ndiye ambaye maisha yake karibu yote yamekuwa ya kupanga.

 

Anapanga kwenye apartments za gharama kweli. Aliwahi kuishi Sinza kwenye mjengo mmoja matata, akaona hapamfai akaenda Makongo kwenye apartment za kishua tu lakini nako akaona kama si hadhi yake. Akahamia Masaki.

Hii yote ni jeuri ya fedha. Anazurura kwenye kumbi mbalimbali kwa sababu pesa ipo. Ingekuwa haipo, pengine angejituliza zake nyumbani. Hapa ndio kwenye msingi wa makala yangu.

 

Uwoya anapaswa kutambua thamani ya maisha yake ya ujana. Atambue kwamba hizi fedha anazipata na kutumbua kuna wakati zitaisha. Yawezekana akawa anapa fedha hizo kwa sababu ya uzuri wake, yawezekana anapata fedha hizo kwa sababu ya ujana wake lakini anatakiwa kujua upo wakati zitatoweka.

 

Ajifunze kupitia mifano ya mastaa wenzake akiwemo muigizaji Wema Sepetu ambaye mpaka sasa bado anahangaika ili kuweza kusimama kwenye nafasi yake. Wema alijua kuchezea fedha sana wakati wake.

 

Alijua kutumia kwenye kumbi mbalimbali za starehe na marafiki lakini yupo wapi sasa?Waswahili wanasema majuto ni mjukuu. Huu ni wakati ambao Uwoya anatakiwa kujitambua na kutumia vizuri fursa aliyonayo.

Kwa njia yoyote ile anayotumia kupata kipato hicho basi ajitahidi kuwekeza maana kuna leo na kesho.Matumizi yasiyokuwa na ulazima ya nini? Watu wanaomzunguka na kumuita Madam ndio haohao baadaye watakaa kando na kuanza kumsema vibaya.

 

Sasa hivi wanamchekea lakini baadaye watamsema vibaya kwa watu.Uzuri siku zote una mwisho. Soko lake huwa ni fupi sana. Jitahidi kuwekeza kwenye biashara au hata nyumba.

Kuliko kuwa mpangaji kwa nini usiwe mama mwenye nyumba hata mbili au tatu mjini?

Mamilioni unayoyachezea huoni kwamba yanaweza kujenga nyumba?

 

Kupanga ni kuchagua, hatuwezi kukulazimisha sana zaidi ya kukushauri kabla mambo hayajaharibika. Ukiona yafaa waweza chukua ushauri la haifai, endelea kutumbua ujana tutakutana uzeeni.

MAKALA: MWANDISHI WETU

#LIVE: MKUTANO MKUU wa YANGA, MSOLA, MWAKALEBELA, SENZO na WANACHAMA…

Leave A Reply