The House of Favourite Newspapers

Isabela asaula live hotelini

0

Isabella Mpanda (3)Isabela Mpanda ‘Bella’ akiwa amesaula.

Mwandishi Wetu

Miss Ruvuma 2006 ambaye pia ni msanii wa filamu za Kibongo na muziki wa kizazi kipya, Isabela Mpanda ‘Bella’, ametoa kali ya kufungulia mwaka baada ya hivi karibuni kusaula nguo zote alizokuwa amevaa mbele za watu.

Isabella Mpanda (2)…akionesha “figure” yake.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, tukio hilo lisilo na staha, lilitokea ndani ya hoteli moja maarufu iliyopo maeneo ya Oyster Bay jijini Dar ambapo inaelezwa kuwa msanii huyo na wenzake, walikuwa wakirekodi video mpya ya mwanadada huyo ‘chakaramu’.

Isabella Mpanda (1)“Unajua mnapokuwa ‘location’, mkimaliza kucheza ‘scene’ moja mnaingia vyumbani kubadilisha nguo kwa ajili ya kuendelea na zoezi la kurekodi. Sasa Bella badala ya kuingia chumbani, yeye aliamua kuvua nguo mbele za wasanii, madairekta na wapiga picha waliokuwa wakishuti video yake.

“Alivua moja baada ya nyingine, tukabaki tumepigwa na butwaa,” kilisema chanzo chetu na kuongeza kuwa kitendo hicho kilisababisha wasanii wenzake aliokuwa nao hotelini hapo kuingilia kati ambapo walimponda kwa kukosa staha.

Risasi Mchanganyiko lilimvutia waya Isabella ambapo alipopatikana alisema:
“Mimi naishi maisha yangu, hakuna mtu wa kunipangia nini cha kufanya. Nilikuwa nashuti video ya wimbo wangu wa Nimekumisi, we elewa tu hivyo,” alisema Isabela.

Leave A Reply