The House of Favourite Newspapers

Jide, Nameless wazua gumzo

0

Jide (1) Mbongo Fleva, Judith Wambura ‘Jide’ na msanii wa muziki wa kizazi kipya toka nchini Kenya, David Mathenge ‘Nameless’ wakikumbatiana.

Mwandishi Wetu

PICHA yenye pozi la kimahaba kati ya Mbongo Fleva, Judith Wambura ‘Jide’ na msanii wa muziki wa kizazi kipya toka nchini Kenya, David Mathenge ‘Nameless’ imezua gumzo kubwa kiasi cha wadau wao kusema wana wasiwasi wawili hao wako kimapenzi huku kesi ya talaka ya Jide ikishika kasi mahakamani, tembea na Risasi Jumamosi.

Kwa mujibu wa picha hiyo ambayo licha ya gazeti hili kurushiwa na chanzo chake lakini pia ipo kwenye mitandao ya kijamii, Jide na Nameless wamegandana utadhani ni sehemu ya kazi yao!

Jide (2)Jide.

MWONEKANO WA JIDE
Picha inamwonesha Jide kwa nyuma akiwa ‘vere klozi’ na jamaa huyo. Mikono ya Jide, wa kulia umemshika jamaa hadi shingoni na wa kushoto umeshika ukuta kwa mbele kuonesha kwamba, alikuwa akijizuia la sivyo wangeanguka. Kidevu cha Jide kimelalia bega la kulia la Nameless.

nameless-kenya-5Nameless

MWONEKANO WA NAMELESS
Kwa upande wa Nameless, yeye amemkumbatia Jide kwa mikono yote iliyokutanikia kwenye mgongo wa Jide na kumfanya aonekana amemmiliki vilivyo msanii huyo. Kidevu chake kinaonekana kikiwa sambamba na bega la kulia la Jide.

JideWALIVYOFANYA WADAU
Baada ya kusambaa kwa picha hiyo, baadhi ya wadau wa Jide au kwa lugha nyingine mashabiki, waliisukuma kwenye Mtandao wa WhatsApp wa mume waliyetangana naye, Gardner G. Habash kwa lengo la kumwonesha picha hiyo ili kumrusha roho.

MITANDAONI GUMZO
Saa chache baada ya kuingia mitandaoni, picha hiyo ilizua gumzo kubwa huku kila mtu akizungumza lake. Kuna ambao walimtakia heri kama ni kweli wana uhusiano huku wengine wakisema si rahisi kwani Nameless ana mke wake (Wahu, mwanamuziki).

RISASI JUMAMOSI LASAKA UKWELI
Juzi, gazeti hili lilimtafuta kwa njia ya simu Jide mwenyewe kwa lengo la kumuuliza kama kuna kitu zaidi kati yake na Nameless lakini hakuwa hewani. Hata hivyo, watu wake wa karibu walisema mwanamuziki huyo yupo nchini Kenya kikazi.
Gazeti hili likajiongeza kwa kumtafuta mmoja wa viongozi wa Jide kwa sasa ambaye aliomba hifadhi ya jina lake na kumuuliza kama anajua chochote kuhusu picha hiyo ambapo alisema:

“Ninavyojua mimi Jide alikuwa Kenya kikazi na huyo jamaa (Nameless). Jide, si Nameless tu, pia amefanya kazi na Morgan Heritage na wamefanya na Sauti Sol. Haiwezi kuwa kweli maana Nameless ana mke.

Risasi Jumamosi: “Kama kweli ni kazi, ni ngoma gani wamefanya Jide na Nameless?”
Kiongozi: “Details hizo (maelezo) hatuwezi kutoa kwa sasa lakini ndiyo wamefanya kazi na wote katika Studio ya Bruce Othiambo ya Sauti Sol.

“Hata mimi mwenyewe nilikuwa Kenya na Jide lakini tumerudi. Kama humpati kwa simu labda amezima, hajaamka kwa uchovu wa safari.”

GARDNER SASA
Risasi Jumamosi juzi lilimtwangia simu Gardner kwa lengo la kumsikia anasemaje kuhusu ‘mtalaka’ wake huyo na Nameless lakini simu yake iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa. Hata alipotumiwa meseji kwa simu na kuambiwa kila kitu, hakujibu.

MADAI YA TALAKA
Wakati hali ikiwa hivyo, gazeti hili lina taarifa ya ile kesi yao ya talaka ambapo habari zinasema kuwa, Jide ameshinda kesi hiyo baada ya Mahakama ya Mwanzo Manzese/Sinza kukubali ombi lake.

Inadaiwa kuwa mahakama hiyo ilitoa hukumu hiyo mwishoni mwa mwaka jana.
Hata hivyo, wiki iliyopita, Gardner alitafutwa na kuulizwa kuhusu ishu ya talaka ambapo alisema: “Hakuna talaka iliyotoka. Kama ingetoka kweli, lazima mimi ningeitwa mahakamani. Sasa mbona sijaitwa?”

Lakini pamoja na utetezi huo wa Gardner, kiongozi mmoja wa Jide alipoulizwa, alikiri kutolewa kwa talaka hiyo mahakamani akisema, anachotakiwa kufanya Gardner ni kufuata kopi yake kwa makarani wa mahakama hiyo.

HABARI NYINGINE
Pamoja na yote, kuna habari kwamba, Jide yuko huru kwa sasa kufuatia shauri lake na mtalaka huyo kuhusu mgawanyo wa mali kumalizika kwenye Ofisi za Ustawi wa Jamii, Kinondoni jijini Dar.

Ilidaiwa kuwa, katika shauri hilo, Gardner aliamua Jide ndiyo agawanye mali kwa kadiri atakavyoona yeye, hata kama hatampa angalau meza ya chakula. Hata hivyo baada ya kauli hiyo, ilipaswa wanandoa hao wakutane ili kuhitimisha safari yao ya ndoa jambo ambalo bado halijafanyika.

Leave A Reply