The House of Favourite Newspapers

Ishu ya Onyango, Daktari Simba Ipo Hivi

0

BEKI kisiki wa Simba, Joash Onyango, amefunguka kuwa kwa sasa anasubiri kuonana na daktari kwa ajili ya kujua siku ya kurejea uwanjani.

Onyango alipata majeraha kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga ambapo Simba ilikubali kichapo cha bao 1-0.

Akizungumza na Spoti Xtra, Onyango alisema: “Namshukuru Mungu naendelea vizuri ila bado sijaanza mazoezi na timu.

“Tangu timu irudi kutoka Dodoma kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji sijaonana na daktari ila natarajia kuonana naye leo (jana) ili aniambie ni lini nitaanza mazoezi na timu.”

~~LEEN ESSAU, DAR

Leave A Reply