ISHU YA TANASHA KUJIFUNGUA…OFM watinga kimafia nyumbani kwa Diamond

BAADA ya tetesi kusambaa mitandaoni kuwa mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Dimond Platnumz’ amepata mtoto wa nne kwa mpenzi wake wa sasa, Tanasha Donna Oketch huku picha zinazodaiwa kuwa ni za mtoto huyo wa kiume zikisambazwa, Kikosi Maalum cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers kiliibuka kimafia nyumbani kwa staa huyo kutaka kujiridhisha.

Awali, baada ya mitandao kutawaliwa na habari hizo, licha ya kuwa suala hilo siyo la uovu, Risasi Jumamosi lililazimika kuwatuma mapaparazi wa OFM ambao wana mafunzo maalum ya kupenya kwenye matukio ya namna yoyote ile.

Mapaparazi wetu wa OFM walitinga moja kwa moja nyumbani kwa Mondi, Mbezi Beach jijini Dar na walipokaribia, walichora ramani kabla ya kufika kabisa getini.

Uchunguzi wa harakaharaka uliweza kubaini kwamba nyumba hiyo ina kamera kila kono hivyo kuwalazimu mapaparazi kutoingia ‘front’ wote.

Mapaparazi wetu walijipanga kwenye ‘engo’ tofauti ambapo wengine walikaa kwa mbali na wengine waliisogelea nyumba hiyo.

Wale waliokuwa mbali ambao walikuwa hawajaingia kwenye himaya ya kamera hizo, walikuwa wakiwafotoa wale ambao walikuwa wameingia kwenye himaya ya kamera za nyumba hiyo.

Mbinu za kikachero zilifanikiwa kukutana na mmoja wa watu wa karibu na familia ya Mondi ambaye alishawishiwa na kukubali kufunguka ukweli kuhusu suala la Tanasha kujifungua.

OFM: Wewe ni ndugu yetu, sisi hatutakutaja popote hebu tuambie kwanza Tanasha na Mondi wapo ndani?

Mtu huyo: Tanasha na Mondi wote hawapo, wametoka…ila nyie bwana msije mkanitaja mtakuwa mmeniharibia.

OFM: Hatuwezi kukutaja sisi hatujawahi mtaja yeyote anayetupa habari.

Mtu huyo: Sawa, kwani zaidi mnataka kujua nini?

OFM: Tumeona tu madai mengi mitandaoni, tumefika hapa ili kujiridhisha Tanasha ameshajifungua au bado?

Mtu huyo: Kumbe hilo tu, sikieni niwaambie ukweli na muondoke fasta nisije kutwa hapa…

OFM: Tawire tawire…

Mtu huyo: Tanasha bado hajajifungua japo ni wa leo wa kesho.

OFM: Unataka kutuambia tumbo ni kubwa sana sasa hivi eeh!

Mtu huyo: Hapana, Tanasha ana tumbo zuri, sio lile la kujionesha kiivyo lakini nakwambia hivyo kwa sababu tayari ameshafika muda wa kujifungua.

OFM: Ok tunashukuru kwa ushirikiano wako, acha sisi tuondoke haraka.

Mtu huyo: Haya karibuni tena, akijifungua tu mimi nitawaambia maana nipo hapa na nitakuwa wa kwanza kujua hilo.

OFM: Tunakuaminia!

Tanasha raia wa Kenya na Mondi ambao penzi lao lilichipukia mwishoni mwa mwaka jana, walikutana na kuanzisha uhusiano ambao muda wowote unakwenda kuzaa matunda kwa kupata mtoto.

Kwa Tanasha yeye ndio mtoto wake wa kwanza kwa Mondi lakini msanii huyo ana watoto wengine watatu aliowapata kwa wanawake tofauti.


Loading...

Toa comment