The House of Favourite Newspapers

Ishu ya ‘Unga’: Wema Alivyoripoti Kituo Kikuu cha Polisi Dar (Pichaz)

 

Gari alilofika nalo Wema Sepetu Kituo Kikuu cha Polisi, (Police Central) Dar.

Wema akitoka nje ya lango kuu kuelekea katika chumba maalum cha mahojiano.

….Akijadiliana na askari kanzu.

Wema na askari kanzu wake akiongozwa kuelekea ofisi nyingine kituoni hapo. 

MSANII wa Bongo Movie, Wema Sepetu ni miongoni mwa wasanii 9 waliotajwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakituhumiwa kujihusisha na mtandao wa biashara haramu ya madawa ya kulevya na kutakiwa kuripoti katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar.

Wema na askari kanzu wake akiongozwa kuelekea ofisi nyingine kituoni hapo.

Wema pamoja na wasanii wengine kama TID, Babuu wa Kitaa na Nyandu Tozi wameripoti kituoni hapo mapema leo wakiitikia wito wa RC Makonda.

Wema aliingia kituoni hapo kimya kimya na kwa kufichwa hivyo kufanya wanahabari wasimgundue, baada ya waandishi wa habari kulalamika kwanini mshtakiwa apitishwe mlango wa nyuma wakati wengine wamepitia mbele, ndipo kamera zikamnasa akiongozana na askari polisi mwanamke aliyeonekana akimpa kampani wakati wa kutoka.

 

Wanahabari wakiwasubiri wasanii mbalimbali wakati wakiripoti Kituo Kikuu cha Polisi Dar, mapema leo.

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Comments are closed.