The House of Favourite Newspapers

Yanga Yajigongea 4G kwa Stand United

KLABU ya Yanga imeifunga Klabu ya Stand United bao 4-0 na kuendelea kujikita kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara. Mchezo huo ulipigwa katika Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Yanga yamefumgwa na Donald Ngoma (dakika ya 17), Simon Msuva (dakika ya 26), Obrei Chirwa (dakika ya 45 kipindi cha pili) na Nadir Haroub Cannavaro (dakika ya 69).

Yanga sasa imefikisha pointi 49 mbele ya watani wao wa jadi, Simba ambao wanapointi 45.

KIKOSI CHA YANGA
1. Deougratius Munishi ‘Dida’
2. Juma Abdul
3. Mwinyi Haji
4. Nadir Haroub
5. Kelvin Yondani
6. Justice Zulu
7. Simon Msuva
8. Thabani Kamusoko
9. Donald Ngoma
10. Obey Chirwa
11. Haruna Niyonzima
Akiba
Ben Kakolanya
Ramadhani Kessy
Vicent Andrew
Deus Kaseke
Martin Emmanuel
Said Juma Makapu

Dk1: Tayari mchezo umeanza kati ya Yanga na Stand United katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Dk 3: Obrei Chirwa anaondoka, anakosa bao la mapema kabisa hapa.

Dk 4: Yanga wanapata kona, anakwenda kuipiga Niyonzima lakini inakosa matunda.

Dk 5: Kanavaro anakosa bao tena.

Dk 6: Msuva anaondoka lakini anapoteza mpira

Dk 7: Juma Abdul anamchezea rafu mchezaji wa Stand hapa, inapigwa faulo kuelekea Yanga

Dk 8: Msuva anapiga kichwa langoni mwa Stand lakini kipa anaokoa.

Dk 10, Shambulizi jingine wanafanya Yanga kwa mpira wa faulo wa Mwinyi lakini Stand wanaokoa

DK 14, Kila upande unafanya mashambulizi lakini ulinzi unaonekana kuwa mkali zaidi kwa kila upande

Dk ya 17: GOOOOOOOOOOAL,Yanga wanapata bao la kwanza baada ya Donald Ngoma kumalizia kwa kichwa krosi ya Simon Msuva. Stand hawajapata kitu.

Dk 19: Chirwa anakoswa bao tena hapa.

Dk 22: Chidebele anaondoka lakini anapoteza mpira huu.

Dk 25: Stand wanakosa bao hapa, wanafanya maamuzi siyo sahihi. Inakuwa kona kuele

Dk 26: GOOOOOOOOOOAL, Simon Msuva anaiandikia Yanga bao la pili baada ya kumalizia pasi ya Donald Ngoma. Stand United hawajapata kitu.

Dk 28: Yanga wanakwenda kama nyuki kulisakama langop la Stand Unite kama nyuki.

Dk 32: Serembe anaondoka anaachia mkwaju baada ya kupokea pasi ya Chedebele lakini kipa dida anaondoa mpira ule.

Dk 33: Cheklembe, Yondani na Dida wanagongana hapa, wote wako chini wamelala.

Dk 38: Tayari mpira unaendelea hapa, Dida anapiga mbele huku kumtafuta Ngoma.

Dk 43: Stand wanaondoka, wqanaingia kwenye penalt box lakini wanaotea.

Dk 43: Chirwa anaondoka, shambulizi la kushtukiza hapa lakini wachezaji wa stand wanagongana hapa na mpira unakuwa kona kuelekea Stand. Tayari kona imepigwa lakini stand wanaondoa mpitra huo.

Dk 45: Zinaongezwa dakika 4.

Dk 45+ 2: Golikipa wa Yanga, Dida anagongana temna na mchezaji wa Stand, mpira unasimama na Dida anatibiwa uwanjani.

Dk 45 +3: Chidebele anakosa bao hapa, anaachia mkwaju unapita sentimita chache kutoka langoni mwa Yanga.

MPIRA NI MAPUMZIKO

Dk 45: tayari kipindi cha pili kimeanza.

Dk 45: GOOOOOOOOOOAL,  Yanga wanapata bao la tatu baada ya Chirwa kuwachambua mabeki na kipa wa Stand United.

Dk 47, Selembe anaingia vizuri kabisa baada ya kugongeana na Chidiebere lakini Disa anatoka na kudaka

Dk 49: SUB, Stand wanafanya mabadiliko, Chidebele anatoka nje

Dk 50: Chirwa anaumia hapa,

Dk 56: Yanga wanafanya mabadiliko, Niyonzima anatoka baada ya kuumia na nafasi yake inachukuliwa na

Dk 57:Yanga wanapata penati baada ya Msuva kuangushwa ndani ya 18. Mulilo analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Msuva

Dk 58: Msuva anakosa penati baada ya kupaisha.

Dk 59: Revocatus Richard anapigwa kadi ya njano baada ya kuchezea.

Dk 62: Yanga wanafanya mabadiliko, Vicent Andrew Dante  anaingia ndani kuchukua nafasi ya Kelvin Yondani.

Dk 63: Ngoma anaumizwa na kutolewa nje kwa machela pengine kwa kuwa alikuwa nje kwa muda mrefu akiuguza majeraha.

Dk 64: Tayari mpira umeshaanza.

Dk 68: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOAAAAAL, Canavaro anaipatia Yanga bao la nne baada ya kupiga kichwa kufuatia kona maridadi iliyochongwa na Juma Abdul.

Dk 75: Stand wanafanya mabadiliko, Mohamed Makala anatoka, anaingia Sebastian Stanley.

Dk 79: Msuva anaingia anaachia mkwavu lakini kipa anaokoa.

Dk 82: Juma Abdul anampasia Msuva, anaingia langoni mwa Stand lakini anakosa.

Dk 84: Stand wanazinduka wanalisakama lango la Yanga, lakini wanakosa muunganiko mzuri wanapoteza hapa.

Dk 87: Chirwa anaingia, anabaki yeye na kipa lakini anakosa bao la wazi kabia.

Dk 90: Dakika 4 zimeongezwa.

Dk 90 +3: Yanga wanapata kona lakini inakosa matunda.

MPIRA UMEKWISHA

 

PICHA ZOTE NA MUSA MATEJA | GLOBAL PUBLISHERS

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Comments are closed.