The House of Favourite Newspapers

Izzo Business: Bado niponipo sana

0

izzo biznez (1)Stori: Boniphace Ngumije

MWANAMUZIKI wa Hip Hop ambaye kwa sasa ameunda kundi lake linalojulikana kwa jina la The Amaizing ambalo yupo pamoja na mwanadada Abela Music, amefunguka kuwa kwa sasa hana mpango wowote wa kujiingiza kwenye ndoa kwa sababu mambo yake mengi bado hayajakaa kwenye mstari, yuko bize kuyaweka sawa ukiwa ni msingi wa maisha yake ya baadaye.

Akipiga stori na Risasi Jumamosi, Izzo alipoulizwa kuwa ataoa lini alifunguka kuwa bado yupoyupo sana na kwamba wakati muafaka ambao Mungu amempangia aoe ukifika basi atafanya hivyo.

“Unajua ndoa ni suala ambalo humjia mtu automatic, so kwa upande wangu bado sijalipa nafasi kubwa sana katika akili yangu kwa sababu nakomaa kuhakikisha biashara yangu ya muziki na mambo mengine vinakaa vizuri ili nikizama kwenye maisha hayo nimudu kasi ya maendeleo,” alisema Izzo.

Leave A Reply