The House of Favourite Newspapers

Jack Pemba Afanya Birthday ya Kufuru…

UGANDA: Mfanyabiashara maarufu nchini aliyehamishia makazi yake nchini Uganda, Pedeshee Jack Pemba, jana alifanya birthday ya kufuru nchini Uganda, huku mwanamuziki mahiri kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Koffi Olomide akiwa ndiye mgeni rasmi.

Jack Pemba (kushoto) akiwa na Koffi
Jack Pemba akimzawadia minoti Koffi

Vipande vya video zilizosambaa mtandaoni, vinamuonesha Koffi akipafomu live wimbo wa Ekotite (Selfie) akiwa na bendi yake, ambapo Jack Pemba anamtunuku noti kibao za dola miamia, na kushangiliwa na ukumbi mzima.

Pemba na Koffi

Kabla ya kufanyika kwa birthday hiyo, awali video ya Koffi aliyojirekodi akiizungumzia birthday hiyo na kuahidi kwamba atakuwepo nchini Uganda, ilikuwa gumzo kubwa mitandaoni na tukio la jana limewaacha wengi midomo wazi kwani si rahisi kwa msanii kama Koffi, kukubali kwenda kupafomu kwenye birthday na hata akikubali, dau lake huwa si la mchezo.

Comments are closed.