The House of Favourite Newspapers

Jackline Mengi: Nimezuiwa Kufika Kwenye Kaburi la Mume Wangu

0

MKE wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Kampuni za IPP Media, Jacquiline Ntuyabaliwe amelalamika kuzuiwa yeye na watoto wake kutembelea kaburi la hayati mume wake, Reginald Mengi.

 

Bila kusema ni nani anaowazungumzia, kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika; “Nimenyamaza kwa mengi sana tu. Mmefikia hatua ya kunizuia mimi na wanangu kuingia kwenye kaburi la mume wangu.”

Ameendela na kuandika “Tunafukuzwa eti mpaka tuombe ruhusa ya kuingia kwenye kaburi la mume na Baba wa watoto wangu. Nimechoka, sitakubali kuendelea kuona wanangu wakisononeka na sitakaa kimya.”

Reginald Mengi ambaye alikuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP alifariki dunia Mei 2, 2019 na kuacha mke (Jacqueline Mengi) na watoto wanne ambao ni Regina, Abdiel, Jayde na Ryan. Watoto hao amezaa na Mercy Mengi pamoja Jackline Mengi.

Leave A Reply