The House of Favourite Newspapers

Jamaa azidisha ‘dozi’, aanguka, afa

0

STORI: Dustan Shekidele, Wikienda
Morogoro: Janga la kitaifa! Wakati wasanii wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ na Rashid Makwilo ‘Chid Benz’ wakiteswa na madawa ya kuleva ‘unga’, jamaa aliyefahamika kwa jina la Halid Bitebo, mkazi wa Kaloleni Kata ya Mji Mpya Manispaa ya Morogoro, anadaiwa kuzidisha ‘dozi ya unga’ kisha kuanguka na kufa.

Akizungumza na Wikienda, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo lililojiri maeneo hayo wikiendi iliyopita, Waldi Mkami alisema: “Ilikuwa saa 12:00 asubuhi, vijana wawili wapita njia walitugongea na kutujulisha kuwa nje ya nyumba yetu kuna kijana (teja), amezidisha dozi ya madawa kisha ameanguka.

“Kweli tulipotoka tulimshuhudia akiwa ameshakata roho ndipo tukatoa taarifa kwa mwenyekiti wa mtaa wetu Mwajuma Ndege.”
Kwa upande wake mwenyekiti huyo, alikiri kutokea tukio na kwamba ndiye aliyetoa taarifa polisi.
Kabla ya polisi kufika eneo la tukio, mwanahabari wetu alizungumza na kijana Waziri Rashid ambaye alidai kumfahamu vyema jamaa huyo.

“Huyu ni teja na shughuli zake ni kuokota vyuma chakavu. Kila siku tulikuwa tunamkanya aache kubwia unga, umeona sasa ameanguka na kufa huku udenda ukimtiririka, kwa vyovyote alikuwa amezidisha dozi,” alisema Rashid.

Leave A Reply