The House of Favourite Newspapers

Jamani Kaka Cheni …Ndiyo Nini Sasa?!-21

1

ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:
Kabla sijamaliza kusema, ghafla mlango ulisukumwa bwana…

“Haa! Baby tumefumaniwa…Mungu wangu jamani…” nilisema hata kabla sijamwona huyo aliyesukuma mlango…
SASA SHUKA NAYO MWENYEWE…

Wote, mimi na kaka Cheni tulikaa kitandani huku mimi nikitafuta kanga yangu na kujifunika kifuani. Tulikaza macho mlangoni lakini hatukumwona mtu…
“Bro, atakuwa nani?” nilimuuliza.
“Sijui, ngoja nitoke nje,” alisema kaka Cheni.
“Nyau,” paka alilia ndani chumbani kwa kaka Cheni. Tuliangaliana na kucheka sana. Kumbe ni paka bwana ndiye aliyesukuma mlango.
Kaka Cheni alitoka kitandani, akaenda kumfukuza kisha akafunga mlango kwa funguo kabisa.
Mimi bado mapigo ya moyo hayakukaa sawasawa kwani nilijua tumefumaniwa na watu wawili. Kama si baba, basi ni mama. Majirani sikuwafikiria sana. Hakuna jirani mwenye uwezo wa kuingia ndani bila hodi, tabia hiyo ni ya mama zaidi.
“Baby ngoja nitoke,” nilimwambia kaka Cheni, akanizuia eti nisitoke kwanza ule ndiyo muda wa kula raha katika maisha yetu.
“Siko sawasawa hata kidogo. Moyo unadunda bado. Mwili uko kama umeteguka, sasa nikisema niendelee kuwemo humu nitakuboa tu sweet…”
“Mi wala hutaniboa,” alisema kaka Cheni na kunikumbatia kwa nguvu zake zote. Nasema nguvu zake zote kwa sababu alinibana sana mpaka nikahisi navunjika mifupa.
Kaka Cheni aliniomba tulale lakini bila mchezo, nikakubali. Tulilala wote. Mimi niliangalia ukutani, yeye akaniangalia mimi.

Kusema ukweli hadi leo hii nikikumbuka nakosa jibu la moja kwa moja kwamba tulikuwa tunajiamini nini! Tulipitiwa na usingizi wa fofofo. Wa kukoroma alikoroma wa kugugumia alifanya hivyo.
Kuja kushtuka, ni saa kumi jioni kwa mujibu wa saa ya kwenye simu yangu…
“Sweet,” nilimwita kaka Cheni, naye akashtuka na kuitika…
“Unajua sasa ni saa kumi jioni?”
“Kweli? Ina maana tumelala zaidi ya saa nne? Si tumelala kuanzia saa sita mchana?”
“Ndiyo maana yake.”
“Lo! Hapa tujiangalie sana. Si ajabu mama au baba wamekuja, wamegonga mpaka wamechoka na wamekaa hapo nje,” alisema kaka Cheni.

Ni kweli hata mimi nilikubaliana naye kwamba, ilitakiwa kuangalia mazingira ya nje kwanza.
Kaka alitoka kitandani, akavaa bukta, akatoka nje. Ukimya uliniambia hakukuwa na mama wala baba.
Mara, kaka Cheni aliingia ndani akakaa kitandani huku akipigwa mwayo…
“Una njaa baby?” nilimuuliza kaka Cheni…
“Sana, kapike chakula bwana.”
Nilitoka, nikaenda jikoni kuandaa chakula. Ni cha mchana ingawaje ilikuwa jioni. Nilipika ugali na samaki wa kukaanga ambao walishakaangwa ilikuwa ni kuwapasha moto tu.

Mimi nikiwa jikoni, kaka Cheni alikuwa bado chumbani. Wakati natoka nilimwacha amelala kwa kujitupa, njaa hiyo!
Baada ya chakula kuiva, nilikiingiza chumbani kwake badala ya sebuleni…
“Amka ule msosi mume wangu,” nilimkaribisha chakula kaka Cheni.
Aliamka, chakula niliweka kwenye stuli. Tukakaa kitandani wote, nikamnawisha nikanawa lakini naye alinawa. Nikaanza kumlisha kama mtoto wangu…
“Kula baby…kula ushibe,” nilimwambia kaka Cheni.
Tulikula chakula wote, tulipomaliza nilitoa vyombo, nikarudi chumbani kwa kaka Cheni. Hapo ikumbukwe kwamba tangu kutoka chumbani kwangu asubuhi sikurudi tena.

“Sweet tukaoge sasa halafu tulale au unasemaje?” nilimshauri kaka Cheni…
“Yaani umeniwahi, nilitaka kukwambia hivyohivyo,” naye alisema.
Nilimshika mkono akasimama akiwa bado ndani ya bukta. Ile tunafika mlangoni tu, demu wake anaitwa Rozimina akaingia…
“He! Mtu na kaka yake mmeshikana mikono kulikoni?” aliuliza Rozimina huku uso wake ukionesha maswali kibao na wasiwasi pia. Maana mimi nilikuwa ndani ya kanga moja tu! Kaka Cheni bukta tu halafu tunatoka chumbani. Hata ungekuwa wewe ungefikiria vibaya.
“Kwani we’ unafikiria nini?” nilijikausha na kumuuliza Rozimina…
“Nyie ndiyo mnajua, mimi nitafikiria nini? Cheni,” Rozimina alisema kisha akamwita jamaa yake…
“Unasemaje?”
“Mlikuwa mnafanya nini na sista ‘ako chumbani?”
“Rozimina swali gani hilo kwa dada yangu?” kaka Cheni alimjia juu.

“Dada yako ndiyo mnatoka chumbani hivyo Cheni. Angalia bukta yenyewe ilivyo, hebu we dada mtu jiangalie nywele. Hakyamungu vile nyie mlikuwa mkifanya tendo baya sana…lakini wewe Cheni huyu Eva si mdogo wako!”
Nilianza kuhisi Rozimina anaweka kiwingu, nilimwangalia kwa hasira sana, nikamwambia…
“Hivi wewe Rozimina kama sisi ni wapenzi wewe inakuhusu nini? Si sisi wenyewe…sasa kwa taarifa yako hatuachani.”
“Ha! Eva, unakiri kutembea na kaka yako? Huoni aibu? Cheni…ama kweli we kiboko…nakuja kumwambia baba yenu,” alisema Rozimina akitoka huku akilia kwa kwikwi…
“Rozimina…we Rozimina,” kaka Cheni alimuita, hakuitika…
“Sista unajua atakuja kusema kweli kwa baba…”
“Aseme, ana ushahidi gani?”
“Si vile ulivyomjibu…”
“Ah! Aende zake huko.”
Mara, tukamwona Rozimina anarudi akiwa ameshikiliwa mkono na mama…

Je, nini kiliendelea? Usikose kusoma wiki ijayo.

1 Comment
  1. eliza says

    nice

Leave A Reply