The House of Favourite Newspapers

Bella aukubali muziki wa Eto Dunia

0

BELLA

Christian Bella‘Obama

Christian Bella‘Obama’ amefunguka kuwa anaukubali uwezo wa mkali wa Bendi ya Amani Kwanza, Eto Dunia hivyo ana kila sababu ya kuhudhuria uzinduzi wa albamu yao iitwayo Pembe Nne za Ulimwengu.maxresdefault

Eto Dunia

Eto anayeunda bendi hiyo na mrembo wa nguvu, Luundo Dunia wamewaomba mashabiki wa Dansi kufika kwa wingi katika Ukumbi wa Mango Garden Kinondoni jijini Dar Ijumaa hii (Machi 25) kwani mbali na shoo yao baab’kubwa, Jahazi Modern Taarab na FM Academia watakuwepo kuupamba usiku huo.

“Mimi na Luundo tutapiga nyimbo zetu kali kama Hapa Kazi Tu, Mvua na Dawa ya Penzi. Yaani Bella mwenyewe ambaye ni Mfalme wa Dansi Bongo atakubali muziki wetu. FM Academia nao wataimba nyimbo zao bila kusahau Jahazi chini yake Mzee Yusuf nao watashusha sebene kali,” alisema Eto.

Leave A Reply