The House of Favourite Newspapers

Jamani Kaka Cheni …Ndiyo Nini Sasa?!-23

0

ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:
Tulipanda kitandani kwa kaka Cheni. Tulikuwa tunavuta kasi ya msisimko kwanza,  nje dirishani kwake tukasikia mtu amekanyaga bati likatoa mlio.
SASA SHUKA NAYO MWENYEWE…


Kuna mtu amekanyaga bati kaka Cheni,” nilimwambia kwa sauti ya sikioni.
“Ni kweli,” na yeye alinijibu.
Tulijua mtu amekanyaga bati kwa sababu nje ya dirisha la kaka Cheni chini kuna bati lilifunikiwa matofali. Sasa baada ya matofali kuondolewa, bati liliendelea kubaki palepale.
“Atakuwa nani?” nilimuuliza nikiwa nahema kwa kasi.
“Sijajua,” alinijibu kaka Cheni.
Tulikuwa tumekumbatiana tukaachiana, tulikuwa tumelala kwa kuangaliana, tukalala kuangalia juu.
“Isijekuwa baba,” nilimwambia kaka Cheni…
“Labda.”
Nilianza kumwona kaka Cheni kama mwanaume asiye na ujasiri kwani alichotakiwa kuniambia ni kunipa neno la kunipa moyo na si kuniongezea wasiwasi. Angeniambia ‘hapana, hawezi kuwa baba, labda kibaka tu’ ningemwelewa kuliko kusema labda.
Nilitaka kutoka kitandani ili kwenda dirishani kuchungulia nje lakini kaka Cheni akanishika mkono na kunirudisha nilale vilevile…
“Lala,” aliniambia.
“Sasa tutajua ni nani?”
“Mimi nimekwambia sijui.”
Mara tukasikia ishara ya mtu kuhema. Ilionekana alikuwa amesimama dirishani kabisa.
“Muulize we nani?” nilimwambia kaka Cheni.

“Hapana, acha tuone mpaka mwisho wake. Itajulikana tu wala usiwe na wasiwasi.”
“Da! Anatukata stimu huyo mtu, natamani iwe ndoto, awe ni kibaka na si baba wala mama,” nilimwambia kaka Cheni.
Kule kuhema kulipotea kidogo lakini haikuonekana kuwa huyo mtu ametoka dirishani kwani angekuwa ametoka lazima angetembea na bati lingelia.
Licha ya kuwa katika hali hiyo, kaka Cheni alileta mkono wake hadi akashika nido zangu na kuzichezeachezea lakini mi mwenzake wala! Hapo nilikuwa nawaza aibu ya mbele yangu.
“We kaka Cheni huoni kuwa ni hatari kwetu? Kwa nini tusikae tukawaza namna ya kujinasua kwanza?”
“Cheni,” sauti ya kike iliita kwa mara ya kwanza tangu tuanze kusikia mishemishe za nje. Alikuwa yule demu wa kaka Cheni, Rozimina.

Kaka Cheni hakutaka kuitika, akaniminya mimi kwa nguvu kama vile kunifinya…
“Usiseme chochote kile mpaka aondoke mwenyewe. Saa hizi anakuja kufanya nini, tena bila taarifa…”
“Ndiyo nashangaa na mimi,” nilishadadia mimi maana simpendi kabisa huyo msichana. Yaani nilihisi kama anakuja kuniletea kauzibe kwa kaka Cheni…
“We Cheni…Cheni,” alizidi kuita.
Alipoona kimya kimetawala akaamua kugonga dirisha kabisa…
“Ngo ngo ngo ngooo!”
“Nyamaza kimya sista,” kaka Cheni alisemea masikioni mwangu ambapo naamini nilisikia mimi tu.
“Yaani Cheni upo ndani halafu hutaki kunifungulia mlango siyo? Sawa bwana.”
Tukasikia akitembea kutoka kwenye eneo hilo lakini cha ajabu, baada ya sekunde tukasikia akigonga kwenye dirisha langu huku akiita…
“We wifi…wifi…wifi.”
Nilikasirika sana. Nilitamani nimtokee hukohuko na kumpa maneno yake ili akome kabisa.
“Baby, unamsikia huyo mtu wako?” nilimuuliza kaka Cheni.

Afadhali safari hii niliweza hata kumuita baby kwani moyo wangu ulitulia baada ya kubaini si baba wala mama aliyekuwa akitembeatembea nje ya dirisha…
“Yaani wifi hata wewe unanifungia vioo, sawa bwana,” alisema Rozimina na kuondoka zake.
Lakini nilimwambia kaka Cheni kwamba, huenda Rozimina hajaondoka basi amesimama nje akisubiri lolote…
“Mpuuzi yule, mimi sitoki na wala wewe usitoke. Yeye anadhani mimi napatikana tu wakati wowote ule. Alitakiwa kuja kwa kutumia mawasiliano.

“Sasa itakuaje?” nilimuuliza huku nikigeuka na kulala nikimwangalia yeye wakati yeye bado alikuwa amelala akiangalia juu. Nilimpapasapapasa sehemu ya kifuani ili kumwamsha hisia zake kwangu japokuwa nilijua bado alikuwa nazo…
“Itakuaje nini sasa?”
“Hatujui kama kaondoka au bado yupo. Kitanda kikicheza si itajulikana tuko wote na nini kinaendelea?”
“Ah! Achana naye yule bwana. asituvurugie mambo yetu.”
Kauli ya kaka Cheni ilinipa ujasiri mkubwa sana, nikaanza naye mimi mwenyewe. Niliinuka, nikamwegemea vizuri, nikamchezea kwa kumgusagusa kama najaribu mwili wake una joto la kiasi gani!
Wote tulibadilika, tukaleta akili zetu pale kitandani, tukahamasishana mpaka tukaingia uwanjani.

Tulijiachia bwana, kwa raha zetu. Sisi ndiyo sisi hakuna mwingine. Mpaka kipindi cha kwanza tunaingia mapumzikoni hakuna aliyeshughulika na Rozimina ili kujua kama aliondoka au bado alikuwa pale na kama alikuwa yupo, ilikula kwake maana tulikidhibiti kitanda kisitoe ushirikiano kwa mtu aliyekuwa nje ya chumba.
Baada ya hapo tulilala kwa ahadi ya kuamshana ikifika saa sita ili tuhamie chumbani kwangu kama tulivyokuwa tumekubaliana.

Lakini tulilala mpaka tukajikuta tunashtuka kukiwa kumepambazuka…
“Ha! Baby, kumekucha,” nilisema nikikurupuka na kutoka kitandani.
Nilifungua mlango na kuingia chumbani kwangu na kujitupa. Hata kabla sijaanza kupitiwa tena na usingizi wa asubuhiasubuhi, mama aliwasili. Alinigongea, nikatoka, nikamsalimia, akaingia ndani kwake.
Kulikucha kabisa, jua lilichomoza, mama alirudi msibani akisema mazishi ni siku hiyo kwa hiyo akasema kaka Cheni aende baadaye.
Ile mama anakata ukuta tu, mimi nilitoka mbio mpaka bafuni, nikatapika sana huku nikimwita kaka Cheni. Safari hii ilikuwa siyo kawaida, kwani na kizunguzungu juu…
“Sista vipi tena..! Eee? Vipi sista?”

Nini kitaendelea? Usikose kusoma wiki ijayo.

Leave A Reply