The House of Favourite Newspapers

Jamani Kaka Cheni …Ndiyo Nini Sasa?!-24

0

ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:
Ile mama anakata ukuta tu, mimi nilitoka mbio mpaka bafuni, nikatapika sana huku nikimwita kaka Cheni. Safari hii ilikuwa siyo kawaida, kwani na kizunguzungu juu…
“Sista vipi tena..! Eee? Vipi sista?”
TAMBAA NAYO MWENYEWE…


Natapika,” nilimwambia kaka Cheni nikiendelea kutapika.
“Unajisikiaje kwani?”
“Kichefuchefu kaka Cheni…tumbo kama linavurugika hivi…”
“Mh! Mimba?”
“Nahisi hivyo kaka Cheni,” niliamua kumjibu hivyo moja kwa moja kutokana na nilivyokuwa najisikia…
“Hee! Sista inaweza kuwa kweli? Itabidi kutoa,” alisema kaka Cheni nikamwona kama adui wa familia yangu kwani kwa kipindi hicho katika kitu nilichokua nahitaji ni mtoto.
“Ha! Kaka Cheni, nitoe mimba?”
“Una maana gani? Yaani uzae na mimi?”
“Ubaya uko wapi?”
“Mh! Sista unaumwa na hauko sawasawa?”
“Niko sawasawa.”
Hapo kidogo sasa nilikuwa nimeacha kutapika. Nikawa nahema tu huku nikitweta kwa kasi ya ajabu. Nilihisi maumivu ya tumbo ya kupita kawaida.
Kaka Cheni alinisimamisha na kunipeleka chumbani kwangu huku akinipa pole.

Ile anatoka tu, hajamaliza mlango, mama akaingia…
“Wewe chumbani kwa dada yako unaingia kuchukua nini?”
“Shikamoo mama…dada alikuwa anatapika kule bafuni ndiyo nikaenda kumchukua na kumrejesha ndani,” nilimwambia…
“Nini tena, malaria ama nini?”
“Mimi sijui mama.”
Mama aliingia chumbani kwangu akasimama akiwa amejishika kiuno…
“Unasumbuliwa na nini binti yangu?”
“Tumbo mama.”
“Tumbo linafanyaje?”
“Linasokota.”
“Ndiyo ukatapika?”
“Ndiyo mama.”
“Linakata?”
“Limekuwa kama limevurugika!”
Mama alinipa pole, akaenda nje na kumwita kaka Cheni…
“Kamtafutie dawa dada yako. Nenda dukani kawaambie anaumwa tumbo la kuvurugika na anatapika.”
Kaka Cheni hakutumbukiza neno lakini najua akili zilikuwa si zake kwa wakati huo. Yeye alikuwa hataki mimi nizae na yeye na mimi sikuwa nalilia kuzaa na yeye bali nilikuwa nalilia kuwa na mtoto bila kujali baba ni nani.
Kaka Cheni akiwa ameondoka, alinitumia meseji…
“Hiyo mimba lazima tuitoe sista. Ni hatari sana kwetu.”
“Hakuna hatari yoyote kaka, we unahisi hatari iko wapi?”
“Ukiulizwa mimba ni ya nani utasemaje?”
“Si nitakutaja!” nilimtania tu hapa ili nimsikie atasemaje!
Hakujibu meseji hiyo bali alinipigia simu lakini sikupokea maana mama aliingia na kunipa maagizo…
“Mimi nimekuja tu kuwaona, narudi msibani. Kama tumbo litachachamaa nipigie simu nirudi nikupeleke hospitali mwenyewe.”
“Sawa mama.”
Alipoondoka tu, nilimpigia simu kaka Cheni…
“Hivi wewe una akili kweli au ni kichaa tayari kwa sababu ya kutapika mara moja tu?”
“Kwa nini baba kijacho wangu?”
“Haa! Nani baba kijacho wako sista?” alinijia juu sana.

“Si wewe.”
“Weee…weee! Koma. Sasa nakwambia kwamba nikirudi nakupiga mangumi tumboni mpaka kitoto chako kife.”
Sauti ya kaka Cheni haikuashiria kwamba anatania kwani alikuwa akihema kwa kasi za hasira.
Mimi niliamua kukata simu na kuanza kutafuta mbinu mbadala za kuhakikisha kaka Cheni hapati nafasi ya kunikaribia hata kwa mita moja toka nilipo.

Baada ya kama nusu saa alirudi akiwa ameongozana na Rozimina…
“Mambo wifi yangu, nasikia unaumwa?”
“Si sana kiasi cha kuja kujuliwa hali,” nilimjibu kwa hasira. Lakini nilijua kaka Cheni hana ubavu wa kumweleza kwamba huenda nina mimba…
“Zaidi nini?”
“Homa tu…”
“Ya matumbo?”
“Eee,” nilimjibu mbovumbovu nikitamani nimwambie aondoke chumbani kwangu. Hapo alikuwa amekaa kitandani mimi nimelala si kwa kuumwa, bali kwa uchovu wa usiku kucha na kaka Cheni kitandani.
“Shika maji na dawa zako,” kaka Cheni aliniambia kwa mkato huku akinipa glasi yenye maji kama aliyetaka kunisusia…
“Sasa baby mbona unampa dawa mgonjwa kwa hasira?” Rozimina alimuuliza kaka Cheni.
Kwa mara ya kwanza tangu nimeanza kumjua Rozimina ndiyo nilimwona ni mtu mwema kwangu siku hiyo tu na dakika hiyo tu. Lakini alinikera kumwita kaka Cheni baby.
Nilikunywa maji, nilipomaliza nikamshukuru na kumrudishia glasi maana alikuwa amesimama akiisubiri…
“Asante sweet,” nilimshukuru.

Rozimina alishtuka sana, akaniangalia kisha akamwangalia kaka Cheni…
“He! Kumbe nyie ni mtu na sweet wake?” aliuliza…
“Ubaya uko wapi? Kwani neno sweet maana yake nini?” nilimpaka maneno Rozimina…
“Mimi najua sweet ni watu wanaopendana…”
“Kwa hiyo mimi na kaka yangu tunachukiana siyo?”
“Mtajua wenyewe lakini siyo kumwita sweet. Mi nadhani wewe wifi unanifanyia makusudi flani hivi, nimekuona tangu majuzi.”
Kaka Cheni alikuwa tayari nje amepeleka kikombe kwa hiyo malumbano yetu alikuwa anayasikia lakini kwa mbali.
Ghafla akaingia, akaja kitandani nilipolala huku akisema kwa sauti ya juu…
“Sista mimi nakuua…nakuua kweli,” akaanza kunipiga mangumi ya tumboni…
“Ha! Baby… nini tena? Kutupiana kwetu maneno wala hakuna uzito wa wewe kuchukua hatua ya kumpiga dada yako mangumi ya tumboni kiasi hicho,” alisema Rozimina huku akimshika mkono kaka Cheni ambaye aliniachia…
Nililia huku nikimwangalia kwa hasira, nikamwambia ukweli kutoka moyoni…
“Narudia tena kaka Cheni, nasema sitoi hata uniue.”

Je, unajua nini kiliendelea hapo? Rozimina alijua dada wa Cheni hatoi nini? Usikose kusoma wiki ijayo

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, INGIA NA LIKE PAGE YA FACEBOOK YA ERIC SHIGONGO===>https://www.facebook.com/shigongotz/

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA TUFOLLOW

INSTAGRAM===>https://www.instagram.com/globalpublishers/

TWITTER===>https://twitter.com/GlobalHabari

FACEBOOK===>https://www.facebook.com/GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE===>https://www.youtube.com/user/uwazi1

Leave A Reply