The House of Favourite Newspapers

Jambazi Sugu wa Magari Akamatwa Akitorokea Uganda

Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limemkamata mtu mmoja aitwaye Peter Thomas Nyanchiwa, anayedaiwa kuwa ni jambazi sugu baada ya kuiba gari na kutaka kutoroka nalo kwenda kuliuza nchini jirani ya Uganda.

 

Akizunumza na wanahabari jijini Mwanza leo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shanna amesema kuwa mtuhumiwa huyo na wenzake wawili, wanadaiwa kuiba gari aina ya Toyota Coaster lenye namba za usajili T 122 DLY mali ya Ismail Abdallah mkazi wa Mwanza.

 

Inadaiwa siku ya tukio hilo, mtuhumiwa na wenzake walikodi gari hilo kuelekea Bunga za Serengeti mkoani Mara kwa madai kuwa wanakwenda kubebea watalii waliokuwa wameharibikiwa gari njiani wakati wakitalii.

 

Ismail aliafikiana na watu hao kisha kuanza safari hadi eneo la Nata Serengeti ambapo mtuhumiwa na wenzake walimfyatulia risasi kwenye taya na kudondoka chini, waliamini kuwa tayari amekufa hivyo wakaanza safari ya kuelekea Mkoani Geita kwa kupitia Barabara ya Bariadi, Shinyanga hadi Kahama kwa lengo la kulipeleka gari hilo Uganda kuliuza.

 

Taarifa za wananchi zilisaidia kufanyika kwa msako na kufanikiwa kukamata gari hilo katika poli la Runzewe mkoani Geita pamoja na Bastola yenye namba H44780Y ikiw ana risasi 12 ndani ya magazine.

 

Sahanna amesema mtuhumiwa na wenzake watafikishwa mahakamani muda wowote upelelezi utakapokamilika huku hali ya Ismail ikiezwa kuwa inaendelea vizuri baada ya wananchi kumkimbiza katika Hospitali ya Wilaya ya Serengeti kutibiwa.

Comments are closed.