The House of Favourite Newspapers

James Rodriguez Atua Bayern Munich

0
Mchezaji wa Real Madrid, Mcolombia, James Rodriguez akiwa ndani ya jezi ya Bayern Munich.

STRAIKA wa Real Madrid, Mcolombia, James Rodriguez ameondoka kwenye kikosi hicho baada ya kutua Bayern Munich kwa mkopo wa miaka miwili.

Kutokana na usajili huo, sasa atakutana na kocha wake wa zamani, Carlo Ancelotti ambaye ni bosi wa Bayern Munich. Licha ya mkopo huo, kuna kipengele kinachoeleza kuwa Bayern inaweza kumsajili Rodriguez kwa jumla ya pauni milioni 31, ambapo katika mkopo wa sasa watatoa pauni milioni 9.

Mchezaji huyo alikuwa akiwindwa kwa ukaribu na vigogo wengine wa Ulaya wakiwemo Manchester United. Ancelotti ndiye aliyemsajili Rodriguez wakati akiwa kocha wa Madrid kwa pauni milioni 63 mwaka 2014 lakini akashindwa kung’ara.

Leave A Reply