The House of Favourite Newspapers

JANUARY MAKAMBA MGENI RASMI KONGAMANO LA WAZALENDO

0
Shaka Ssali.

WAKATI siku zikiyoyoma kuelekea Septemba 2, mwaka huu katika kongamano la kihistoria lijulikanalo kama Meza ya Wazalendo litakalofanyika ndani ya Ukumbi wa Nkurumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, imefahamika kuwa mgeni rasmi siku hiyo atakuwa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, Mheshimiwa January Makamba.

Januari Makamba.

Akizungumza na Ijumaa, mratibu wa kongamano hilo kutoka Taasisi ya Vijana Wazalendo wa Kitanzania, Tanzania Youth Patriots (TYP), Vian Nchimbi alisema kuwa, siku hiyo ratiba itaanza rasmi saa 7 mchana hadi saa 11 jioni ambapo mbali na uwepo wa Makamba, pia atakuwepo mtangazaji maarufu duniani kutoka Kituo cha Redio cha Sauti ya Amerika (VoA), Shaka Ssali katika kulipamba kongamano.

Eric Shigongo.

“Mgeni rasmi katika kongamano hili la kihistoria anatarajiwa kuwa heshimiwa January Makamba atakayesindikizwa na watoa mada mashuhuri nchini, akiwemo Lawrence Masha, Eric Shigongo, Maria Sarungi Tsehai, Mzee Shaba na Benjamin Fernandes,” alisema Vian na kuongeza;

 

Lawrence Marsha.

“Njooni kwa wingi ili muwe sehemu ya mjadala mpana ambapo mambo mbalimbali juu ya Utanzania wetu na dhana nzima ya uzalendo kwa jumla yatazungumzwa. Wanafunzi wa sekondari, vyuo vya elimu ya juu, taasisi mbalimbali na wananchi wote mnakaribishwa kwani kiingilio ni bure kabisa.”

Maria Sarungi.

Kwa mawasiliano zaidi, unaweza kupiga simu au ujumbe wa SMS au WhatsApp kupitia namba 0769984781.
Kongamano hili limedhaminiwa na Clouds Media Group na Global Publishers.
MIMI NI MZALENDO, NITAHUDHURIA, WEWE JE?

STORI: MWANDISHI WETU, DAR

Usipitwe na Matukio, Install ===>Global Publishers App

Leave A Reply