The House of Favourite Newspapers

JATU Yapelekwa Takukuru, Waziri Bashe Ataka Hatua Kali Zichukuliwe

0
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe

WAZIRI wa Wizara ya Kilimo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hussein Bashe ameagiza kuipeleka katika Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) Kampuni ya Jenga Afya Tokomeza Umasikini (Jatu) katokana na madai yaliyotolewa na wawakilishi wa wakulima dhidi ya viongozi wa JATU.

 

Hili limekuja baada ya wakulima kutoa fedha zao kwaajili ya kulimiwa mashamba yao na kampuni hiyo lakini kazi haikufanyika kama inavyotakiwa, mwezi wanne mwaka huu Waziri Bashe aliunda kamati kwa ajili ya kukagua mashamba yanayodaiwa kulimwa na kampuni hiyo kwa ajili ya wakulima waliotoa fedha zao, hofu imetanda miongoni mwa wakulima wanaodai kupoteza mabilioni ya fedha katika kampuni hiyo.

 

Waziri Bashe akizungumza jijini Dodoma na baadhi ya wanachama wa kampuni hiyo kuhusu madai hayo, alisema walichokiona kiko nje ya uwezo wao, hivyo wanawakabidhi ripoti Takukuru.

“Mahali ilipofika hili jambo kwetu sisi Wizara ya Kilimo it’s over and above (tumefika mwisho na liko juu yetu). Ndiyo maana leo nimeongea na DG (Mkurugenzi) wa Takukuru nikamwomba watu ili sisi tukabidhi tulichopata,” alisema Bashe.

JATU inaelezwa kuwa imefunga Ofisi zake katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma

“Tumekubaliana na DG wa Takukuru ataongea na IGP (Mkuu wa Jeshi la Polisi), ataongea na Financial Intelligence Unit wote watakutana na kuunda timu”.

 

Pia alieleza kusikitishwa na Menejimenti ya JATU kufunga ofisi ya Morogoro, Dar es Salaam na Dodoma akisema wamehamia Rukwa.

 

Imeandikwa: John Mbwambo kwa msaada wa mitandao.

Leave A Reply