The House of Favourite Newspapers

Jay Moe: Msiba wa Ngwair Sikulia Kama wa Langa

0
Jay Moe.

MKONGWE asiyechuja kwenye muziki wa Hip Hop Bongo, Juma Mchopanga ‘Jay Moe’ amefunguka kuwa alipofariki msanii mwenzake Ngwair alijikaza na akafanikiwa kutolia lakini alipofariki Langa, alimwaga machozi.

Langa enzi za uhai wake.

Akipiga stori na Showbiz Extra, Jay Moe alisema ingawa Ngwair alikuwa ni mshkaji wake wa karibu lakini siku ya msiba wake, alijikaza ila alipofariki Langa alishindwa kujizuia kutokana na msanii huyo kufariki siku chache baada ya kumueleza kuwa ameacha madawa ya kulevya.

Ngwea enzi za uhai wake.

“Nilikuwa na mvutano na marehemu Langa kwa muda mrefu kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya, siku chache kabla ya kifo chake alinieleza kuwa yupo poa na ameacha unga.

“Alinitaka tufanye kazi ya pamoja, hata hivyo tukiwa hatujakamilisha mpango huo nikapokea tarifa za kifo chake, kwa kweli nilumia sana,” alisema Jay.

NA ALLY KATALAMBULA | GAZETI LA AMANI

NUH Atoboa Siri Kuachana na Mkewe Shilole Atajwa

Leave A Reply