The House of Favourite Newspapers

JAYJAY: Nililazimishwa penzi nikanasa mimba!

0

JINA lililoanza kuzoeleka midomoni mwa wadau wengi wa sanaa ya filamu Bongo ni Jayjay, lakini cheti chake cha kuzaliwa kimeandikwa Janeth Jackson.

Kwa sasa anafanya kazi ya uigizaji na miongoni mwa filamu ambazo amefanya vyema ni pamoja na Who Is My Child? na nyinginezo kibao ambazo ameonesha uwezo wa hali ya juu.

Mwandishi wetu Brighton Masalu alikutana naye na ‘kumbananisha ukutani’ kwa kumuuliza maswali kumi ya nguvu ambapo alifunguka mambo mengi. Fuatilia hapa chini…

Ijumaa: Ni kitu gani ambacho hukunyima raha maishani mwako?
Jayajay: Ni kitendo cha kukosa malezi ya mama, huwa naumia mno.
Ijumaa: Pole, ilikuwaje?

Jayajay: Baba na mama walitengana nikiwa na miaka miwili, hivyo niliendelea kuishi na baba, nilimuona mama nikiwa na miaka 16, hata hivyo alifariki muda mfupi baada ya kufahamiana.
Ijumaa: Pole sana, unafanya nini nje ya sanaa ya uigizaji?
Jayjay: Ahsante, mimi ni mjasiriamali lakini uigizaji ndiyo ndoto ya maisha yangu.
Ijumaa: Nini siri ya urembo wako?

Jayajay: Kupenda usafi, natumia losheni ya kawaida (anaitaja jina) na kujipenda, basi.
Ijumaa: Vipi, una mpenzi, mchumba au ni mke wa mtu?
Jayajay: (Anatazama juu na kukunja uso kidogo), hapana, kwa kweli sina hisia tena na mapenzi, nimeshaumizwa mno, siyataki hakuna mwenye mapenzi na mimi.

Ijumaa: (kwa shauku kubwa), kwa nini? Hebu nisimulie kidogo.
Jayjay: Nilianza kuyachukia mapenzi tangu siku ya kwanza naanza kuyafanya. Siku ya kwanza kufanya mapenzi, nililazimishwa (alibakwa) na siku hiyohiyo nikanasa mimba.
Ijumaa: Pole sana, kwa hiyo una mtoto?

Jayjay: (Kwa tabasamu hafifu), yeah, anaitwa Very Nice, nampenda sana binti yangu, japo nilimpata katika mazingira magumu.Ijumaa: Ni eneo gani la mwili wako ambalo likiguswa na mpenzi wako unahisi kuchizika?
Jayajay: Hilo ni siri yangu ila nikishampata mwenye mapenzi ya kweli kwangu, atanijua vizuri.
Ijumaa: Oke, unakunywa pombe?

Jayjay: Aah, noo….! Siwezi, nimetoka kwenye familia yenye misingi na maadili ya kidini sana, kwa hiyo sijawahi.
Ijumaa: Changamoto zipi umezipitia kwenye kazi hii ya uigizaji?
Jayjay: Changamoto ni nyingi sana lakini kwa kifupi ni za kawaida kwangu na nazikabili ipasavyo.

Leave A Reply