The House of Favourite Newspapers

Je, Umefikia Wakati wa Mitetemo ya Jangwani Kuhamia kwa Farao?

0

Wakati tetesi zikiendelea kusikika kutoka kila kona kuhusu mshambuliaji kinara wa Yanga, Fiston Mayele, sasa Pyramids iko kwenye nafasi kubwa ya kumnasa mshambualiaji huyo baada ya kuishinda timu kutoka huko nchini Saudi Arabia.

Hili pia linathibitishwa kwa kauli ya mtendaji mkuu wa Yanga, Andre Mtine baada ya kusema kwama Mayele hakutambulishwa kwenye kilele cha siku ya mwananchi kwa sababu hayuko kwenye mpango wao kutokana na ofa mbalimbali ambazo wamepokea kutoka timu mbalimbali zikihitaji huduma ya mshambuliaji huyo, Fiston Mayele.

Aidha, wakati hayo yakiendelea, inasemekana kwamba Pyramids wanategemea kumtangaza mshambuliaji huyo mwishoni mwa wiki hii.

Leave A Reply