The House of Favourite Newspapers

Jembe la Gamondi laonywa Daktari Mkuu wa timu Yanga

0
Beki wa kushoto wa Yanga, Joyce Lomalisa

AKIWA nje akiendelea kuuguza majeraha yake ya kifundo cha mguu ‘enka’, beki wa kushoto wa Yanga, Joyce Lomalisa amepewa onyo  hiyo, Moses Etutu.

Beki huyo ameondolewa katika msafara wa timu hiyo, ulisafiri kwenda nchini Ghana, kwenda kucheza mchezo wa tatu wa hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika uliotarajiwa kupigwa jana Ijumaa.

Lomalisa alipata majeraha hayo katika mchezo uliopita wa michuano hiyo, walipocheza dhidi ya Al Ahly ya nchini Misri baada ya kuchezewa vibaya na Percy Tau katika kipindi cha pili kabla ya kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Nickson Kibabage.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Lomalisa ameambiwa na daktari wa timu hiyo, kama anataka kupona haraka basi ni lazima aukanyagie kwa nguvu mguu bila ya kujali maumivu ataakayosikia.

Lomalisa alisema kuwa kuukanyagia mguu huo, kutakwenda sambamba na kufanya mazoezi ya gym na kuchezea mpira, ili majeraha hayo yapone katika enka hiyo.

Aliongeza kuwa anaamini atarejea uwanjani mapema, kwa ajili ya kuipambania timu hiyo, katika michezo ijayo ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Ligi Kuu Bara.

“Majeraha yangu yanaendelea vizuri nashukuru, ninaamini nitarejea haraka uwanjani, hivi sasa ninaafanya mazoezi chini ya uangalizi wa daktari wa timu.

“Nimeshauriwa niukanyagie mguu kwa nguvu, bila ya kujali maumivu nitakayoyasikia, pamoja na kuchezea mpira katika kiwanja cha mazoezi.

“Ninaendelea kufuata maagizo na maelekezo ambayo madaktari wa timu wamekuwa wakinipa huku nikiendelea na matibabu ya dawaa ninayoendelea kuyapata ili nirejee haraka,” alisema Lomalisa.

STORI: WILBERT MOLANDI

Leave A Reply