The House of Favourite Newspapers

Jeuri ya Zuchu Kwa Diamond Platnumz Yawekwa Wazi, Afanya Makubwa Chini ya Lebo ya WCB

0
Zuchu akiwa na bosi wake, Diamond Platnumz.

 

ZUCHU; ni malkia mpya wa muziki nchini Tanzania ambaye ametumia miaka miwili vizuri ndani ya muziki na kujitengezea himaya yake na sasa anatambulika kama msanii wa kike mwenye ushawishi zaidi kimauzo mtandaoni.

 

Mrembo huyo amefanya makubwa chini ya Lebo ya WCB ambapo inasemekana kwa sasa ana jeuri mbele ya bosi wake, Diamond Platnumz kwa sababu mauzo yake yanatisha.

 

Tayari Zuchu amefikisha streams (watazamaji/ wasikilizaji) zaidi ya milioni 70 katika Mtandao wa Boomplay akiongoza Afrika Mashariki upande wa wasanii wa kike.

Malkia mpya wa muziki nchini Tanzania, Zuhura Othman Soud ‘Zuchu’.

 

Mwaka 2020 alifikisha streams milioni 12 na kumfanya kuwa msanii wa kike aliyesikilizwa zaidi kwenye mtandaoni huo kwa mwaka huo.

 

Mwaka 2021 alifikisha streams milioni 37 na kuandika rekodi kama msanii wa kike duniani aliyesikilizwa zaidi kwenye mtandaoni huo.

 

Mwaka 2022 hadi sasa ametoa wimbo mmoja tu wa Mwambieni, lakini tayari amejikusanyia streams zaidi ya milioni 24 hivyo anaongoza Afrika Mashariki upande wa wasanii wa kike.

 

Kwenye mtandao huo, Zuchu ana nyimbo nne zenye streams zaidi ya milioni 10 sawa na Diamond Platnumz au Mondi akifuatiwa na Jovial wa Kenya mwenye nyimbo tatu kisha Rayvanyy na Otile Brown (Kenya) ambao wote wana mbili.

 

Kwa jumla, kwa ujumla wasanii wenye streams nyingi Boomplay Afrika Mashariki ni Diamond, Rayvanny, Mbosso na Zuchu; wote kutoka WCB.

Ikumbukwe Extended Playlist (EP) ya Zuchu ya I Am Zuchu yenye nyimbo saba ilikaa tano bora kwenye chati za Boomplay kwa wiki 75 huku ukishika namba moja kwa wiki 35.

 

Kwa jumla, wasanii wa Afrika wenye streams nyingi Boomplay ni; Burna Boy, Joeboy, Fireboy, Omah Lay, Olamide, Kizz Daniel, Davido na Wizkid, wote kutokea na Nigeria na wakiwa na streams zaidi ya milioni 100 huku Burna Boy akiwa na zaidi ya streams milioni 200.

 

Zuchu tayari amefikisha views zaidi ya milioni 320 kwenye YouTube na kuwa msanii kike namba tano Kusini mwa Jangwa la Sahara kufanya hivyo.

 

Wanaomtangulia ni Sinach (views milioni 654), Yemi Alade (milioni 633), Tiwa Savage (milioni 374) na Ada Ehi (milioni 321), wote hawa ni kutokea Nigeria.

 

Zuchu amekuwao kwenye chati za YouTube nchini Tanzania kwa wiki 109 na ndiye msanii wa kike Bongo aliyekaa kwenye chati hizo kwa muda mrefu zaidi.

 

Kwa sasa Zuchu anashika namba nne kama msanii wa kike Afrika mwenye subscribers wengi YouTube Afrika akiwa nao milioni 1.97, waliomtangullia ni Sherine (Misri) -milioni 4.25, Zina Daoudia (Morocco) -milioni3.07 na Yemi Alade (Nigeria) -milioni 2.0.

 

Video ya wimbo wake wa Nyumba Ndogo iliyotoka Julai 1, 2021, imefikisha views milioni 21 na kuwa video pekee ya Singeli iliyotazamwa zaidi YouTube hivyo kuivunja rekodi iliyokuwa inashikiliwa na Rayvanny.

Cc; @sifaelpaul

SAKATA LA MUME ALIYEMUUA MKE KWA RISASI LAWAIBUA WANAHARAKATI, WAKILI ATAJA HATMA YA FAMILIA

Leave A Reply