The House of Favourite Newspapers

Jezi ya Maradona ya Bao la Mkono wa Mungu Yauzwa kwa Bilioni 17

0
Nyota wa zamani wa Timu ya Taifa ya Argentina Diego Armando Maradona akifunga bao kwa mkono dhidi ya Uingereza

JEZI ya nguli wa soka Duniani marehemu Diego Armando Maradona imeweka rekodi baada ya kuuzwa kwa kiasi cha Euro Milioni 7 kwenye mnada huko nchini Mexico ambayo ni sawa na kiasi cha Shilingi Bilioni 17,150,913,157.

Jezi imeuzwa kwa thamani ya pesa za kitanzania Bilioni 17

Jezi hiyo ndiyo iliyovaliwa na Maradona kwenye robo fainali ya Kombe la Dunia la mwaka 1986 iliyochezwa kwenye Uwanja wa Aztec nchini Mexico kati ya Argentina na Uingereza ambapo Uingereza ilifungwa bao 2-1 huku kumbukumbu mbaya ikiwa ni Uingereza Kutolewa kwa bao la mkono bao ambalo lilipata umarufu mkubwa Duniani kama bao la mkono wa Mungu.

 

Jezi ya nguli huyo wa soka imetoka kwenye mikono ya kiungo wa zamani wa Uingereza Steve Hodge ambaye ndiye aliyebadilishana jezi na Diego Maradona katika pambano hilo ambalo haliji kusahaulika kwenye historia ya mpira wa miguu.

Leave A Reply